Mjumbe wa ZFA Taifa kupitia Wilaya ya
Chake Chake Sharrif Juma Said ametangaza nia ya kujitosa kuwania nafasi ya
Makamo wa Rais wa ZFA Taifa kwa upande wa Pemba katika uchaguzi wa ZFA
uliopangwa kufanyika tarehe 9, April.
Sharrif amesema kuwa ameamua kujitosa kuwania nafasi
hiyo kwa kile anachodai anatosha kushika nafasi hiyo kutokana na kuwa na uwezo
wa kuongoza nafasi hiyo.
Alisema amekuwa mchezaji na kiongozi
wa siku nyingi wa mpira kwa nyakati tofauti na hiyo inampa sifa ya kuchaguliwa
kuwa miongoni mwa viongozi wa awamu ijao ya chama cha mpira wa miguu Zanzibar
(ZFA).
Sharrif anakuwa mwanamichezo wa
kwanza kutia nia ya kuwania nafasi ya makamo wa Rais wa ZFA Taifa Pemba katika
uchaguzi wa mwaka huu ambapo pia nafasi hiyo inategemewa kutetewa na makamo wa
Rais wa sasa Ali Mohammed Ali.
Msikilize Said anavyozungumza katika mahojiano na mwanamichezo wetu kutoka Pemba Is-haq Muhammed
No comments:
Post a Comment