Jezi rangi ya Njano ni timu ya Wawi
Star wakati Mwamuzi Mwadini Ali
akimsikiliza mlinzi wa timu hiyo.
Timu ya Wawi Star yanyakuwa ubingwa
wa ligi daraja la Kwanza Taifa Pemba baada ya jana kufanikiwa kuichapa timu ya
Dangers Boys magoli 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Gombani.
Timu ya Wawi Star inakuwa bingwa
ikiwa imebakiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kucheza michezo minne na
kushinda mitatu na kutoka sare mchezo mmoja.
Kutokana na ushindi huo wa jana
uliowahakikishia kucheza ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba msimu ujao,
mashabiki wa Wawi Star walilazimika kufanya shangwe na vifijo huku wakiondoka
uwanja wa Gombani kwa kidedea hadi walipofika katika makazi yao huko Wawi.
Timu ya Wawi Star katika hatua ya
makundi ambapo ilikuwa kundi la kusini Pemba ilishika nafasi ya pili kwa kupata
alama 33, nyuma ya mahasimu wao Mkungu Malofa waliofikisha alama 34.
Katika hatua ya 6 Bora Wawi imejipatia
jumla ya alama 10, ikifiatiwa na Chuo/Basra yenye alama 6, Mkungu Malofa 5,
Dangers Boys 4, Maji maji 4 na New Star 4.
Mchezo unaotarajiwa kuchezwa leo
katika ya timu ya Mkungu Malofa na Maji maji huenda ukatoa timu nyengine
itakayopanda daraja, huku timu nyingine zikijulikana hapo kesho baada ya mchezo
kati ya Chuo/Basra yenya alama 6 na Maji maji yenye alama 4, na mchezo baina ya
Timu ya Wawi Star na New Star ambayo nayo inajipa moyo wa kupata nafasi hizo.
Timu 3 za juu zilizoingia katika
hatua ya 6 ndizo zitakazopanda daraja kucheza ligi kuu ya Zanzibar msimu ujao.
No comments:
Post a Comment