"KAMPENI YA FICHUA VIPAJI"
Mlinzi wa timu ya IGWEE SPORT CLUB au watoto wa mjini wa Iringo
Musoma Kelvin Deo amesema ingawa changamoto ni nyingi sana katika soka la
Tanzania lakini hatorudi nyuma atapigana mpaka kuhakikisha anazishinda
changamoto hizo zilizombele yake mpaka pale atakapofika safari yake.
Safari hii si safari nyengine isipokua ni safari ya kuyafikia
malengo yake ya kua mchezaji bora wa kitaifa na kimataifa huku akiamini malengo
hayo anaweza kuyafikia pale atakapokua ndani ya Azam fc.
Hayo ameyasema jana wakati alipokua akizungumza na SALMA SPOT’S
MEDIA katika kampeni ya FICHUA VIPAJI
ikiwa ni mchakato wa kuwatembelea, kuwakagua
na kuwaonesha hadharani wachezaji wadogowadogo wenye malengo makubwa na mazuri
katika soka.
Kelvin Deo amesema siku zote amekua akifanya mazoezi ya hali
ya juu kuhakikisha anayafikia malengo aliyoyapanga,amekua akiwasikiliza vizuri
walimu wake na kuyatekeleza kivitendo yale yote anayofundishwa.
Amesema ingawa Tz kuna timu nyingi lakini anaamini anaweza
kuyafika malengo yake ikiwa kama atafanikiwa kuingia Azam kwani ndio timu pekee
inayoweza kumfikisha katika safari ya malengo yake hayo.
Deo anasema “lengo ni kufika mbali kisoka pia kuwasaidia
wadogo wanaochipukia, na ndoto zangu hasa siku moja nitacheza soka katika timu
ya Azam fc kwa jinsi wanavyocheza mpira wa pasi nawakubali sana na hakuna
anaebisha kwa hili”alisema Deo.
Amesema njia pekee ni kucheza katika timu hiyo.
Akizungumzia baadhi ya changamoto ambazo amedai kua ni moja
kati ya vikwazo vya kuzima hamasa za wachezaji amesema “changamoto zipo tena
nyingi, kama ligi tuliyocheza sisi mechi za mwanzo takriban sita tumesafiri
kwenda kucheza nje ya wilaya,mwisho wa siku tunapewa kikombe chenyewe pasipo
viongozi kufikiria gharama tulizotumia,kuna chakula,usafiri na makaazi basi
angalau hicho kikombe kilingane kidogo gharama zake na isiwe sawasawa lakini
kilingane japo kidogo”alisema Deo.
Aidha ameiomba serikali iwe inatoa fungu kwa ajili ya ligi
hata ziwe ndogo kutawanya wachezaji kujaa hamasa ya kucheza mpira kwani ndio wanakotokea wachezaj vipaji pia wawashajihishe
wadhamini kujitokeza na kudhamini kwa wingi timu za mpira hapo mambo yatakwenda
sawa.
Pia ametoa ushauri kwa wachezaji wenzake kujituma kwa hali ya
juu pasipo na kukata tamaa huku wakiamini siku moja mafanikio yatakuja wenyewe .
IGWEE SPORT CLUB ndio tumu bora msimu huu kuwa mabingwa wa
mkoa wa Mara ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa baada ya kuwafunga BARUTI FC
goli 1 kwa 0 katika uwanja wa Karume Mjini
Musoma akiwa mmoja wa wachezaji mahiri waliyoiletea timu hiyo ushindi ni Kelvin
Deo.
Deo ni mlinzi wa kushoto wa timu hiyo mbali na ukabaji mzuri
anaosifika nao lakini pia ni mchezaji mwenye sifa na uwezo wa kucheza nambari
zaidi ya hiyo, anacheza nambari tatu, saba na kumi na moja kwa umakini mkubwa
sana.
No comments:
Post a Comment