"KAMPENI YA FICHUA VIPAJI"
Sembe ni alievaa flana nyekundu na kaptura nyeusi wakiwa na furaha baada ya kumaliza game ya kirafiki BWELEO. |
Mmoja miongoni mwa Mawinga mahiri Zanzibar Sembe Aliy (25) amesema
kuwa lengo lake hasa katika soka ni kuhakikisha siku moja anakua mchezaji
maarufu na mashuhuri katika medani za soka nchini.
Ametoa kauli hiyo ya kusisimua wakati alipokua akizunguza na
SALMA SPORT’S MEDIA leo hii katika kampeni ya “FICHUA VIPAJI” ikiwa ni mchakato
wa kuwatembelea, kuwakagua na kuwaonesha hadharani wachezaji wadogowadogo wenye
malengo makubwa na mazuri katika soka.
Sembe ni mchezaji wa kawaida katika timu za mitaani “BWELEO” Zanziabar amesema siku zote amekua
akijituma kwa mazoezi ya kila aina kuhakikisha siku moja anafikia lengo lake
hilo.
Amesema vipaji vipo vingi Zanzibar lakini vinaishia mitaani
hasa maeneo ya mashamba, hii inatokana na kutothaminiwa kwa wachezaji
wadogowadogo hasa wa vijijini.
Sembe amesema serikali kupitia ZFA waandae kamati ya kukuza vipaji
na kutoa sapota kwa wanasoka wa chini kwani kuna wachezaji wazuri ambao
wakiibuliwa wanaweza kulitangaza taifa vizuri ndani na nje ya nchi.
Sembe ni mchezaji anaemudu vizuri kucheza nambari saba (7) na
kumi na moja (11) mashabiki wengi wa BWELEO wanamkubali kwa kazi yake lakini
mpaka leo hii amebakia mitaani.
SALMA SPORT’S MEDIA imeridhishwa na kiwango chake na iwapo
hatua za kuwaenzi vijana hawa zitachukuliwa kwa hamasa zaidi tunaamini Semba
atailetea sifa nchi kitaifa na kimataifa.
Ndoto zake ni kuwa Super star siku moja lakini mpaka sasa
anaishia katika timu za “maskani” na ukimtazama kiukweli utavutiwa na uchezaji
wake akiwapo uwanjani.
Akizungumzia changamoto anazokabiliana nazo katika soka
amesema kitu cha kwanza kuzaraulika kwa wadau wa soka iwe ngazi zinazofanana au
hata za juu yake.
Sembe amemalizia kwa kusema ataendelea na msimamo wakehuohuo katika mazoezi na kucheza soka kadiri iwezekanavyo
mpaka atakapoyafikia malengo yake huku akiwaomba wadau wa soka nchini kutilia mkazo
na nguvu katika kuwawezesha wachezaji wadogo kwa kuwasapoti na kuwakuza
akiamini wanavipaji vya hali ya juu lakini vinashindwa kuoneakana.
No comments:
Post a Comment