Mchezaji nambari sita (6) wa timu ya Mbeya City team “B” Ligi
kuu Tanzania bara Majdi Shabani Kivuluge
amesema soka la Tanzania linaonekana kukua kiasi fulani tena ni la kuvutia
lakini bado linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo kwa namna moja ama nyengine
zinaweza kurudisha nyuma maendeleo hayo.
Kauli hiyo ameitoa leo hii alipokua akizungumza na SALMA
SPORTS MEDIA juu ya muonekano wa soka la Tanzania ukilinganisha na mataifa
mengine.
Kivuluge amesema soka la Tanzania linakua sana na hii
inasababishwa na timu kua na ushindani mkubwa sana hivyo kila mmoja inampasa
kuonesha ari ya kushinda na ndio maana ikaonekana kukua kwa kiasi Fulani.
“soka limekua kwa kiasi kikubwa sana mana kwasasa Ligi
inaushindani mkubwa sana tofauti na zamani, leo kila timu ina mashabiki wengi na
kila mmoja anajihisi yeye ni mshindi na hakuna anaekubali kushindwa”alisema
Kivuluge.
Akizungumzia upande wa changamoto zinazolikabili soka nchini
ambazo ndizo zinazodhoofisha ukuaji wake mpaka kufikia pale panapo takikana
amesema katika timu nyingi viwanja wanavyochezea ni vibovu havisatahili kabisa
kwa hadhi ya soka.
Pia amesema kuna uzorotaji na uhaba wa wadhamini wa kudhamini
michuano mbalimbali, amesema bila ya kuwepo wadhamini hakutokua na soka imara
ni lazima wajitokeze kusapoti nchi yetu.
“ hebu tazama viwanja ni vibovu na ligi hazina wadhamini wa kutosha, sanasana
unakuta team muda mwingine inaishiwa pesa ya kuwalipa wachezaji unakuta
miezi mitatu mchezaji hajalipwa unafikiri patachezeka mpira apo”alisema
Kivuluge.
Kivuluge amesema ili kuinua zaidi soka nchini ni lazima
wadhamini wajitokeze kwa wingi na serikali ijitahidi kuongeza bidi za
kuwatafuta hapo soka ndipo litakapokua.
Aidha ametoa wito kwa upande mwengine wa kukuza soka kuwa, ni
muhimu sana kuwa na mpango wa kukuza na kuwaendeleza vijana kwani wapo wengi
mitaani na wanavipaji lakini hakuna anaewajali “Viongozi waweke mpango endelevu
wa kukuza vijana kuwe na academic nyingi na kila team Iwe na uwanja wake kama
unavyona kwa Azam fc”. Alisema Kivuluge.
No comments:
Post a Comment