Mchezo wa soka nchini Tanzania unaonekana kuwa bado kukua upo chini ukilinganisha na nchi za wenzetu zinazosifika
kwa maendele ya mchezo huo.
Kauli hiyo imetolewa le na Goalkeepar wa timu ya Makumba fc ligi daraja la pili ngazi ya mkoa Dar es salam Babuu Adinan (De
gea) alipokua akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA juu ya taswira halisi ya soka chini.
Katika mzungumzo juu ya taswira hiyo tulibahatika kuzungumza mengi sana na maongezi yetu kwa uchache
yalikua kama ifuatavyo.
Salma Hassan: unalizungumziaje soka la Tanzania kwa ujumla kiukuaji wake?
Adinan : Soka letu
bado sana ukilinganisha na nchi nyengine za wenzetu sisi bado tupo nyuma
na hali hii inatokana na viongozi wenye dhamana na soka.
Salma Hassan : kivipi viongozi hawa
wanashindwa kuliendesha soka vizuri mpaka tukawa kama wenzetu ambao leo
hii wamekua mfano mzuri duniani?
Adinan : Sababu kuu ni umimi na ubinafsi uliyotawala na si
jambo jengine ingawa yapo lakini hili ni kubwa lao.
Salma Hassan: ok sasa
nini kifanyike ili soka letu likue nasi tuwe kama wengine wenyekutajika?
Adinan : kama viongozi
wataacha hiyo tabia ya umimi na ubinafi tu
soka la bongo litakuwa kwa sababu kuna vipaj vingi vya ukweli na wapenda
soka wapo wengi tu.
Hayo yalikuwa ni mazungumzo kati ya mwandishi wetu wa SALMA
SPORT’S MEDIA pamoja na mlinda mlango wa timu ya Makumba fc wakati tulipokutana
nae na kuzungumzia kuhusu soka letu la Tanzania.
No comments:
Post a Comment