Wednesday, 2 March 2016

MAKOCHA CHAGUENI WACHEZAJI KWA VIPAJI NA SIO KUJUANA.




Hakika hiki ni  kipaji cha kupigiwa mfano nchini mwetu, mafanikio ndio yake dira na malengo mema ndio aliojipangia, mengi sana amekumbana nayo katika soka kama ni changamoto lakini bado anaendelea kuzipembua na kuziweka upande mpaka pale apatakapo afike.

Amedai kua baadhi ya viongozi wa soka nchini huongozwa na maslahi yao binafsi katika utekelezaji wa majukumu katika timu hivyo ikitokea tu kocha huyu kama hakukupenda hata ufanye nini huwezi kuibuka kidedea kwake.

Bila ya shaka unahamu na shauku ya kumjua huyu ninani tunayemzungumzia hapa, si mwengine isipokua ni mchezaji kipaji alieanzia  timu ya  Spark Youth ya Mombasa nchini Kenya Raymond S Nkwande Mdudu.

Huyu ni mtanzania mwenye umri wa miaka 22, alisafiri sana kisoka ndani na nje ya nchi na mengi sana alikumbana nayo katika safari yake hii, kipaji chake ni chakupigiwa mfano laiti kama inatunzwa nuru hii ni lazima ing’are vyema na kumurika nchini zokte katika medali ya soka.

Twende pamoja uone historia fupi kisoka ya mchezaji huyu pamoja na majanga yaliomkuta  kisha njoo na jawabu katika suala hili, inakuaje kama atajaliwa na kuthaminiwa nchi yetu itakua wapi kisoka?

Timu yake ya kwanza aliyowahi kuchezea ni  Chipukizi ya Tabora mnamo mwaka wa 2009 baada ya kuonekana kipaji chake ni kizuri kinakua kadiri ya siku zinavyokwenda basi pia iliamuliwa kuondoshwa timu hiyo na kupandishwa juu kidogo timu ya kanda ya magharib Umiseta katika mwaka 2010.

Hapo pia hali ilikua kama kawaida yake alipaform vizuri  baadae kulipita mchujo wa kutafuta tano bora katika timu hiyo hatimae alifuzu.

Kibaha Kipinguambae ni mdau na mwalimu mzuri wa soka alimuona na akaamua  kumpeleka  katika skuli yake ya  lord Baden Powell 2010 ili kumuendeleza kisoka na kweli alikua.

Hakikaya  uchezaji wake akiwa kiwanjani hufurahisha wengi sana hasa kwa mipira anavyoinasa miguuni mwake kanakwamba Kiwembe kutua katika Sukamu, mwaka 2012 akafanikiwa kuingia Yanga youth kama ni maendeleo makubwa kwake, apo amefanya majaribio ya kutazamwa na mwishowe alikubalika.

Kama kawaida ya mambo mengi duniani huwa na pande mbili ya faida, hasara au changamoto hapa sasa kazi ndipo ilipoanza, madudu mengi yalianza  kuibuka, ubabaishaji ukaanza kisa tu haikua chaguo la mtu fulani machoni mwake ikapelekea kuachwa katika timu hiyo.
Baada ya miezi minne  Mdudu hakurudi nyuma alijaribu tena bahati yake akiamini kipaji alichonacho anaweza kukiendelea na kufikia malengo yake ya kua mchezaji mzuri wa kuitangaza nchi yake ndani na njea, mashabiki wake walimtia moyo kua anaweza na kila kona ilithibitikia kweli kama naweza, alikwenda  Azam Youth Team hapa nasema “asikwambiae  mtu kulikua na watu zaid ya 250 lakini kwa jitihadi niliyoionesha tulibaki watano tu nami ni mmoja wao,  fikiria wanne tu ndio walioruhusiwa  kubakia  camp kasoro mimi tu peke yangu  sjui why” alisema Mdudu kwa huzuni ya kusikitisha akionesha ni namna gani baadhi ya viongozi hapa nchini wanavyoshiriki kwa makusudi kuua malengo ya wenziwao.

Anadelea kueleza “ kulikua na Coach Muhindi Vivec alikua ananiamini sana, mimi striker2 mido2 bek1 sikuletwa na mtu, nlienda try mimi mwenyewe, hata ukiwauliza Azam players leo hii basi  wananijua kwa uwezo wangu, nlikua naitwa Kavumbagu nilikua maarufu sana pale kuzidi hata niliowakuta, huyu Mrundi kavumbagu alikua Yanga.

Mpaka leo hii Raymond S Nkwande Mdudu hajui nini kilicho msibu hapo, ukizingatia kwanini anafaulu vizuri na anakubalika lakini baadae huanza bifu, alichokigundua ni kuwa, kumbe ni ile kuwa juu zaidi kisoka kuliko wenyeweji wa hapo ambao walimu ndio walikua matarajio yao kwa maslahi yao, anasema “kuna baadhi ya viongozi naweza kukutajia wananiambia Coach kasema nisije kumbe ni uwongo mtupu wa kutaka nibakie nyumbani tu ili nionekana mkorofi baadae wapenyeze fitina zao, nikawa nakaa tu home, wachezaji wenzangu wananiambia natafutwa na Coach nikienda anaulza mbona sikuoni siku hizi jibu langu ni kua nimeambiwa nisije kidogo kuna mambo yanarekebishwa hata mwenyewe anashangaa”alisema Mdudu.

Mpenzi msomaji wetu hii ndio Tanzania kisoka unajionea mweyewe hali halisi ya mambo, haya ndio maisha ya kijana huyu katika maendeleo yake ya soka na sasa yupo tu kipaji chake anakiendeleza mitaani lakini bado hajakata matumaini washauri wa mambo walimwambia alikopita alipita sipo hakua na mtu nyuma yake alikua yeye peke yake hata iweje hawezi kuonekana.

Akizungumzia kuhusu wachezaji wa vijijini  Nkwande amesema  vjijini kuna wachezaji wengi  na wazuri sana wakiwezeshwa wanaweza,amesema wanacheza Ndondo na wanafanya vizuri.

“wachezaji hawa wa vijijini  wapatiwe walimu, wapatiwe vifaa hasa mipira imekua tatizo kwao, viongoz waende huko tena waanzie chini shule za msingi, wawape misingi ya soccer vijana wakiwa wadogo”alisema Mdudu.

Amesema amekaa kenya muda mwingi lakini hakuona vipaji vya hali ya juu vya soka kama nchini Tanzania “humu bwana kuna vipaji visi sana lakini ndio ivyo”alisema Mdudu.

Mwisho kabisa amewashauri viongozi wa soccer waache ubabaishaji na kuchagua wachezaji kwa kujuana hapo ndio soccer nchini Tanzania  litakua.

Pia viongozi na wadau wa soka watazame sana vipaji hasa maeneo ya vijiji  kwa sababu vipo vingi lakini havipati nafasi ndio maana hakuna wachezaji wengi walio .

No comments: