Kwa namna yoyote ile Ujerumani na Argentina ni mataifa mawili makubwa kisoka duniani
katika zaidi ya mapambano matatu mataifa haya mawili yamekutana yakiwemo mashindano makubwa kama yale ya Kombe la Dunia huku likikumbukwa lile pambano la fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.
Ligi ya Bundesliga imekuwa na nyota wengi sana kutoka Argentina huku kwa sasa nyota kama Franco di Santo anayekipiga SV Werder Bremen, David Abraham ni mtu muhimu katika ukuta wa nyuma pale Eintracht Frankfurt, Emiliano Insua ameisaidia VFB Stuttgart kuepuka kushuka daraja
Kukiwa na muunganiko wa mastaa kutoka Latin America, wachezaji wengi kutoka Argentina hawakawii kuendana na mazingira ya Bundesliga kwa sababu huchukua muda mfupi tu kabla ya kuanza kuonesha uwezo wao uwanjani.
kama mwenyekiti wa Hamburge SV anavyosema “Wachezaji wa ki- Argentina hawana gharama na wanachukua muda mchahce kuendana na matakwa ya ligi, hawana tofauti na wachezaji wa Ulaya”
Mwanzo Mbaya
Historia ya wachezaji wa Argentina katika Bundesliga haikuanza kwa kutisha sana, yalikuwa ni majira ya kiangazi ya mwaka 1972 ambapo Christian Rudzki na Horacio Neumann walipokuwa wachezaji wa kwanza kutoka bara la America ya Kusini kujaribu bahati yao katika Ligi ya Bundes Nchini Ujerumani
Rudzki alikaa mwaka mmoja na kucheza michezo minne tu akiwa na Hannover 96. Neumann alifanikiwa kucheza michezo 20 katika kipindi cha miaka miwili na nusu akiwa na klabu ya FC Kolon kabla ya kutimkia Ufaransa.
Shujaa wa HSV
Baada ya kipindi cha karne mbili Jose Horacio “Nene” Basuado alitia unyayo wake katika ardhi ya Ujerumani na hapo ndio stori ikaendelea kunoga. Ilichukua kipindi cha miaka mitano kabla hajaiona familia yake kwa mara nyingine lakini Basuado alifanikiwa kutikisa katika ligi ya Bundes akicheza michezo 44 na kufanikiwa kucheza katika fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani wakati huo akiwa ni mchezaji wa Stuttgart
Raia mwenzie wa Argentina Rodolfo Cardoso ndiye Muargentina aliyecheza michezo mingi kuliko mchezaji yeyote yule Kutoka Argentina, katika Ligi ya Bundes alifanikiwa kucheza michezo 220 kwa FC 08 Homburg, SC Freiburg, SV Werder Bremen pamoja na Hamburger SV kati ya miaka ya 1989 hadi 2004.
Bundesliga yawa kivutio
Cardoso alifanikiwa kucheza soka la mafanikio mpaka alipofikia hatua ya kustaafu soka mwaka 2004 tayari Bundesliga akawa kivutio cha mastaa wengi akiwemo Dieo Placente aliyefanikiwa kucheza michezo 171 katika kipindi cha miaka minne alichokaa Buyer Leverkusen
Lakini walikuwa ni VFL Wolfsburg waliofanikiwa kunufaika kwa kiasi kikubwa na huduma za wachezaji kutoka Argentina kwa kipindi hicho. Majina kama kina Andres “Magic Mouse”,D Alessandro, Pablo Quattrocchi, na Diego Klimowicz wote walipatikana katika klabu hiyo ya Wolfsburg
Klimowicz alikwenda na kuwa moja ya wafumania nyavu maarufu katika historia ya Bundesliga akifanikiwa kupachika kambani goli 71 katika michezo 213 akiwa na Wolfsburg,VFL Bochum pamoja na Borussia Dortmund.
Huu ndiyo Muda muafaka sasa
Baadhi ya majina kama kina Javier Pinola aliyekipiga kwa kipindi cha miaka 10 na klabu ya FC Numberg pamoja na Martin Demichelis aliyefaniukiwa kuchukua makombe manne ya Bundesliga akiwa na klabu ya FC Bayern Muchen wanaweza kuwa wameondoka lakini bado kuna idadi kubwa sana ya nyota wengi wa ki-Argentina waliobaki katika ligi kuu ya Ujerumani.
Santiago Garcia amecheza michezo 63 tangu ajiunge na Werdebremen mwaka 2013 wakati huo mchezaji mwenzie wa zamani Alfredi di Santo kwa sasa anawanyanyasa mabeki wa Schalke. Abraham alikuwa moja ya wachezaji wa U-20 wa Argentina walioshinda kombe la Dunia mwaka 2005 akifanikiwa kucheza sambamba na kina Javier Mascherano pamoja na Lionel Messi.
Akiwa amefanikiwa kujiunga na Ligi ya Bundes mwaka 2013, Abraham ndiyo ingizo la hivi karibuni katika orodha ya wa-Argentina waliofanikiwa kukipiga Bundesliga lakini kama Historia inaendelea bila shaka Abraham hatakuwa Muargentina wa mwisho kukipiga Bundesliga.
No comments:
Post a Comment