KAMPENI “FICHUA VIPAJI"
Ili kusifika na kua bora katika soka ni lazima kufanyike
juhudi za makusudi kwa mchezaji mwenyewe kimazoezi huku akinuwiya lengo lake
alilolipanga kulifikia hapo anaweza kuwa juu kama walivyowengine ambao leo hii
tunawasifia kila pembe ya nchi.
Ushauri huo umetolewa
leo na mmoja kati ya Manager wa Stend United FC ya ligi kuu Tanzaniabara Ramadhan Mohammed
alipokua akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA katika “KAMPENI YA FICHUA VIPAJI”
inayowatembelea na kuwakagua wachezaji wadogowadogo na hata kwa wachezaji au
timu kubwa ili kutoa ushauri wa namna gani inavyowezekana mpaka wachezaji wa
chini kuwa juu na hatimae kuliinua soka la Tz kwa ujumla.
Mohammed amesema wachezaji vipaji wapo wengi nchini lakini
wanaoonekana ni wachache, amesema ni lazima kwa wachezaji wadogowadogo
wazidishe bidii katika mazoezi siku moja watatajika tu.
“wachezaji vipaji wapo na wazidishe juhudi tu mpira siku zote ni mazoezi juhudi zao ndizo zitakazo wafanya watoke
kimpira na kulitangaza vyema taifa, nafikir vijana wengi wameona mfano mzuri
kutoka kwa Mbwana Samata,hivyo wazidishe
juhudi na kuzingatia kile wanachofundishwa ndio kitu kikubwa”alisema
Mohammed.
Amesema ili kuinua vipaji vya wachezaji, timu kubwa kubwa
zinatakiwa ziwe na Academy ili wawafunze vizuri vijana, amesema hata TFF hilo
waliwahi kuliona lakini mpaka sasa hafamu utekelezaji wake “nakumbuka TFF
waliweka mikakati endelevu kwa kila timu inayoshiriki ligi kuu kua na team “B”
lakini hilo pia naona hasa kwa team ndogo zinashindwa kufanya hivyo kulingana
na uwezo wao hasa kiuchumi kua mdogo” alisema Mohammed.
Sambamba na hayo amesema soka la Tz kwa ujumla linaonekana
kukua kidogo tofauti na zamani kwa sababu timu nyingi sasa zinaonekana kuwa na
upinzani wa hali ya juu ingawa changamoto zilizopo zinarudisha nyuma juhudi za
wachezaji baadae kutokua kwa kiwango kinachoridhisha.
Mohammed ametaja changamoto kubwa inayozikumba timu nyingi
nchini na kufanya hata soka kwa ujumla kuzorota ni uchumi mdogo waliokua nao
wachezaji na timu zao.
Amesema Lazma team ziwe na vyanzo vya kupatia mapato pia
kutafuta wafadhili na hata watu wanao miliki makampuni wajitoe pia katika soka ili kuweza kusaidia mchezo wa mpira wa
miguu kukua zaidi na zaid.
Mwisho kabisa ametoa wito kwa Serikali kupitia mamlaka husika
, ili kuendeleza na kukuza vipaji kwa vijana kurudishwe michezo mashuleni,
kwenye makampuni yawepo mashindano mbalimbali kama UMISETA na pia zianzishwe
Academy hata kama sio kila mkoa , kila
kanda ipate Academy 2/3
Amesema TFF ikifanya
hivyo anaamini mpira utaendelea
kukua na kutapatikana akina Samata wengi
nchini Tanzania
No comments:
Post a Comment