"KAMPENI YA FICHUA VIPAJI"
Wadau wa soka nchini wametakiwa kupunguza au kuondosha kabisa
SIASA katika medani za soka ili kuruhusu vipaji vya wachezaji kukua.
Kauli hiyo imetolea leo na mchezaji wa Polisi Mara daraja la kwanza Danny Manyenye wakati
alipokua akizunguza na SALMA SPORT’S MEDIA
katika kampeni ya “FICHUA VIPAJI” ikiwa ni mchakato wa kuwatembelea,
kuwakagua na kuwaonesha hadharani wachezaji wadogowadogo wenye malengo makubwa
na mazuri katika soka.
Amesema viongozi wa soka nchini wamekua washabikiaji wa Siasa
mpaka huiingiza katika soka hivyo hupelekea kukinzana baadhi ya mitazamo baadae hutofautiana wao kwa wao hatime
kutokua na maendeleo katika timu husika.
Sambamba na hayo pia Danny amesema Tanzania ina vipaji vingi
sana mitaani lakini wanaotakiwa kuviendeleza hawaonekani na badala yake wanasubiri kumuona anatoka chini mwenyewe kwa
nguvu zake na anaposhindwa ndio humalizika kabisa kisoka.
Katika kutimiza ile kampeni ya “FICHUA VIPAJI” SALMA SPORT’S
MEDIA imeshuhudia umahiri wa mchezaji huyu
mwenye jezi nambari 7 mgongoni na anaecheza nambari 9 na 10 uwezo wake
wa hali ya juu unaonekana.
Sifa kuu iliyogundulika mara tu baada ya kuona uchezaji wake nikwamba
ana mashuti mazito , pasi za mwisho pamoja na kupiga vichwa vya kiufundi.
Kutokana na changamoto zilizopo Danny amesema kama kweli nchi
ina nia ya kua na wachezaji wazuri na taifa litajike hakunabudi kwa wadau wa
soka na viongozi kutoa sapoti kwa timu za mpira,kuwaboreshea mazingira yao hapo
nchi itakua tu kisoka.
No comments:
Post a Comment