Kutokana na
matokeo mabovu iliyoyapata timu ya Tottenham kwenye mechi yao ya ugenini dhidi
ya Borussia Dortmund kocha wake amekiri kuwa waliharibu gemu hiyo.
Mauricio
Pochettino kocha wa timu hiyo amesema “timu yangu haikucheza vizuri kwenye
mechi yetu ya ugenini dhidi ya Borussia Dortmund kwenye michuano ya Europa
League hatua ya 16 bora.”
Alieleza “ni
vigumu kueleze lakini hii ni siku mbaya kwetu na nimesikitishwa sana na kiwango
chetu. Hatukucheza vizuri ndiyo maana tukapoteza game, tunahitaji kupambana
kwenye mchezo wetu wa marudiano wiki ijayo. Kipigo cha bao 3-0 siyo mazuri
kwetu lakini tunahitaji kuendelea kupambana na kujaribu Alhamisi ijayo”.
“Hii ilikuwa
ni mechi yetu ya kwanza kupoteza kwa bao 3-0 msimu huu. Tunahitaji kutulia na
kuhakikisha haijirudii tena”.
Spurs
ilijikuta ikichezea kichapo cha bao 3-0 ugenini huku wachezaji wenye uzoefu
kama Eric Dier, Harry Kane, Mousa Dembele na Erik Lamela wote wakianzia benchi
kwenye mechi hiyo.
Magoli ya
Dortmund yalifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang ambaye alifunga goli la kwanza
kwa kichwa wakati Reus yeye akalipiga msumari jahazi la Spurs kwa kufunga bao
mbili zilizokamilisha ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya wageni Spurs.
Watu wengi
wanajiuliza kwamba, kuwapumzisha wachezaji hao ni kwa ajili ya mechi ya Premier
League kati ya Spurs dhidi ya vibonde Aston Villa?
No comments:
Post a Comment