
Bayern Munich yaambulia patupu ugenini kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la UEFA
Nusu fainali ya pili ya
ligi kuu ya kilabu bingwa barani Ulaya ya UEFA iliwakutanisha Atletico Madrid
na Bayern Munich katika uga wa Vicente Calderon.
Bayern Munich waliokuwa
wakicheza ugenini walikuwa na wakati mgumu kupenyeza kwenye ngome ya ulinzi ya
Atletico Madrid na kushindwa kupata goli.
Wenyeji Atletico Madrid
walileta faraja kwa mashabiki wao kwa kupata goli la pekee lililofungwa na Saul
Niguez katika dakika ya 11 na kuletea ushindi wa 1-0.
Mechi ya marudiano
itachezwa siku ya Jumanne tarehe 3 Mei katika uga wa Allianz Arena nchini
Ujerumani.
No comments:
Post a Comment