
Idumu imekuwa ndio timu ya mwanzo kuondolewa katika kinyang’anyiro cha kucheza ligi kuu ya Zanzibar baada ya jana kukubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Chwaka, katika mchezo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani hapa mjini Unguja.
Timu ya Chwaka jana
imemaliza michezo yake yote ya hatua ya sita bora kanda ya Unguja na kufanikiwa
kuwa vinara wa ligi daraja la kwanza
taifa ikiwa na alama 11, kwani alama hizo hakuna timu yoyote itakazo zifikia
katika ligi hiyo.
Chwaka walianza kupata
mabao ya mapema, ambapo mchezaji Awadh Salum ameweka mabao mawili katika dakika
ya 4, na dakika ya 12, na mnamo dakika ya 29, Suleiman Omar akaipatia Chwaka
bao la tatu.
Kipindi cha pili Chwaka
walionekana kujisahau kabisa na kuridhika na mabao waliyoyapata, ndipo Idumu
wakaanza kuja kwa kasi, na ndipo Othman Khamis akaipatia Idumu bao la kwanza,
na katika dakika ya 80 Idumu wakapata bao la pili lililofungwa na Khamis Haji.
Na mtanange huo
ulimalizika kwa Chwaka kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, na kuwaondoa Idumu
katika kinyang’anyiro cha kucheza ligi
kuu ya Zanzibar msimu ujao wa mwaka 2016 – 2017.
Idumu wamemaliza
michezo yote huku wakiondoshwa katika kinyang’anyiro hicho cha ligi kuu wakiwa
na alama nne 4, na Chwaka wamemaliza michezo yake wakiwa ndio vinara na alama
11, huku wakisubiri kucheza ligi kuu msimu ujao wa mwaka 2016 – 2017.
No comments:
Post a Comment