Timu za FSC ya Kangani na Sharp ya Micheweni leo zimegawana
point baada ya kutoka sare ya kufungana magoli 3-3 kwenye mchezo wa ligi kuu ya
Zanzibar kanda ya Pemba uliochezwa kwenye uwanja wa Gombani.
Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na watazamaji wachache FSC
ndiyo waliotangulia kujipatia bao katika dakika ya 5 lililofungwa na mchezaji
wake Shahal Hassan ambaye alipachika la pili kwenye daki ya 19.
Hata hivyo kutangulia si kufika ndivyo ilivyotokea uwanjani
hapo kwa Sharp Victor kuyarejesha mabao hayo kupitia kwa wachezaji wake Hamad
Ali dakika ya 32 na Khatib Hamad katika dakika ya 39 na kulipeleka pambano hilo
mapumziko timu hizo zikiwa zimefungana magoli 2-2.
Timu zote zilirudi kiwanjani katika kipindi cha pili kwa kasi
huku FSC ikionekana kufuta makosa yake kwa kupanga mashambulizi ya uhakika, na
ndipo kwenye dakika ya 67 walipojipatia goli la tatu lililofungwa na mchezaji
Richard Gritan.
Dakika 2 kabla kumalizika kwa mchezo huo Sharp Victor
ilifanikiwa kusawazisha goli la tatu lilowekwa wavuni na mchezaji wake Khamis
Ali kwenye dakika ya 88.
Na hadi mwisho wa mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Hassan
Gerrei akisaidiwa na Suleiman Juma na Suleiman Kisauti FSC 3 na Sharp Victor.
Katika mchezo mwengine uliochezwa kwenye uwanja wa FFU Finya
timu ya Jamhuri akaiadhibu Aljazira kwa magoli 4-1.
Katika mchezo wa kwanza Jamhuri ilikubali kipigo cha bao 1-0
kutoka kwa Chipukizi, huku Aljazira wakipokea kipigo cha magoli 4-1 kutoka kwa
Kizimbani.
Kesho Jumanne kutakuwa na mchezo mmoja tu kwenye uwanja wa
Gombani, mchezo unatabiriwa kuwa mkali kati ya Chipukizi na Kizimbani.
No comments:
Post a Comment