Timu ya Yanga ya Dar-es Salam ambao ni wawakilishi wa
Tanzania katika michuano ya Klabu bingwa Afrika imewasili visiwani Pemba leo
kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mabingwa wa soka wa Misri
National Al-Ahly utakaochezwa Jumamosi.
Kikosi cha Yanga kikiwa na wachezaji 24 kimewasili kwenye
uwanja wa ndege wa Pemba Airport majira ya saa 10 za jioni kwa ndege tatu
tofauti za kampuni ya Al-Salaam Air na moja kwa moja kuelekea katika Hoteli ya
Pemba Misali Sunset iliyopo nje kidogo ya mji wa Chake Chake.
Timu hiyo itaanza kufanya mazoezi kesho asubuhi katika uwanja
wa Gombani hadi hapo Ijumaa itakaporudi Dar-es salaam kwa mchezo huo.
Yanga imefudhu katika hatua hiyo baada ya kuwatupa nchi timu
ya APR ya Randwa kwa kuilaza mabao 2-1 huko Kigali na mchezo wao waliorudiana
walitoka sare ya kufungana kwa bao 1-1 hivyo Yanga kufanikiwa kuvuka kwa jumla
ya alama 4.
Mwaka uliopita Yanga ilitolewa katika hatua kama hii na timu
ya National Al-Ahly kwa changamoto ya mikwaju ya penalt, baada ya Yanga
kushinda nyumbani kwa goli 1-0 na wao kufungwa kwa 1-0 walipokwenda Cairo
katika mchezo wa marudiano.
No comments:
Post a Comment