Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu ya mpira wa kikapu ya
NBA nchini Marekani Golden State Warriors, wamevunja rekodi ya msruru wa
ushindi wa mechi nyingi zaidi ndani ya msimu mmoja.
Golden State Warriors walishinda mechi yao ya 72 baada ya
kuipindua San Antonio Spurs kwa vikapu 92-86 kwenye mechi iliyochezwa hapo
jana.
Kufuatia ushindi huo, Golden State Warriors iliweza kuvunja
rekodi ya ushindi wa mechi nyingi zaidi ndani ya msimu mmoja wa NBA iliyokuwa
ikishikiliwa na Chicago Bulls.
Katika mechi hiyo dhidi ya San Antonio Spurs, nyota wa Golden
State Warriors Stephen Curry aliibeba timu yake kwa kufunga jumla ya vikapu 37.
No comments:
Post a Comment