KAMPENI "FICHUA VIPAJI"
Timu za Chipukizi na Mwenge ambazo zilikuwa hazijawahi
kufungwa tokea kuanza kwa ligi kuu ya Zanzibar Kanda ya Pemba msimu huu jana
zilionja machungu baada ya kupekea vipigo.
Chipukizi ambazo imeshinda katika michezo yake mitatu ya
kwanza ilijikuta ikilala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Young Islanders katika mchezo
uliochezwa kwenye uwanja wa Gombani.
Young Islanders walitangulia kupata bao katika lakika ya 54
lililofungwa na mchezaji wake Abdulrahman Hassan, hata hivyo mshambuliaji
machachari wa Chipukizi Abdulkarim Ali aliisawazishia timu hiyo katika dakika
ya 70.
Bao la ushindi la Young Islanders liliwekwa wavuni na Salim
Ali Salim kwenye dakika ya 77.
Na hadi dakika 90 za mwamuzi Suleiman Kisauti zinamalizika
Young Islanders 2 na Chipukizi 1.
Katika uwanja wa FFU Finya timu ya Mwenge ya Wete nayo
ikijikuta chali mbele ya timu iliyonekana kibonde kutokana na kushindwa kufanya
vizuri kwenye michezo yake mitatu ya kwanza kwa kupata sare 1 tu Okapi ya Msuka
kwa kuchapwa bao 1-0.
Na katika mchezo baina ya FSC na Aljazira uliochezwa kwenye
uwanja wa Kangani Skuli timu ya FSC imeibuka na ushindi wa magoli 3-1.
Leo ndiyo leo pale viwanja vyote vitatu vitakapowaka moto FFU
Finya kukiwa na Hardrock na Kizimbani, Kangani Skuli itakuwa ni kati ya
Dogomoro na African Kivumbi na Gombani Shaba iliyojeruhiwa kwenye mchezo
uliopita watakuwa na wakongwe Jamhuri.
No comments:
Post a Comment