Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi
Zanzibar (JKU) imeendelea kuonesha ubabe wake na kuzidi kujiweka kileleni mwa
ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja bada ya kuwabamiza Jang’ombe boys mabao
2-1.
Katika mtanange huo uliochezwa ndani
ya dimba la Amani majira ya saa kumi za Jioni JKU walianza kupachika bao katika
dkk ya 36 lililofungwa na Moh’d Abdallah.
Na bao la pili lilifungwa na Emmanuel
Martin mnamo dakika ya 46 ya mchezo huo.
Kwa upande wa Jang’ombe boys bao la
kufutia machozi limewekwa kimyani na Bakar Thani katika dkk za nyongeza za
mchezo huo.
katika mchezo huo mchezaji wa JKU
Khamis Said ameoneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa
Jang’ombe boys Juma Ramadhan.
Akizungumza na SALMA SPORTS MEDIA
kocha wa timu ya Jang’ombe boys Issa Othman Amasha amesema kuwa mchezo ulikuwa
ni mzuri kwa timu zote mbili, “mchezo ulikuwa ni mzuri kwa timu zote mbili ila
JKU wameonesha uzoefu katika mchezo wa leo, tumefungwa kwa sababu JKU ni
wazoefu kuliko wachezaji wangu kwa sababu ni bado wadogo na ni msimu wa kwanza
kuja ligi kuu”.
Aidha Amasha aliendelea kusema,
“Tamaa ya kuelekea nne bora sasa
haipo ila tujitahidi tubakie daraja tu kwa sababu mechi tunapoteza tu pint
tunazo kidogo kuna watu wana point 28, 30 sasa kwa mm siwezi ninaejua mpira
siwezi kusema nina tama ya kuingia nne bora wakati tuna point 18, jitihada
tutaonesha kuhakikisha timu yetu inabakia daraja”.
Pia kocha msaidizi wa JKU Khamis Muhsin nae amesema “mchezo ulikuwa mzuri ila
kutokana na viporo vya apo kwa apo tumecheza juzi tumekuja na leo tunacheza na
kesho kutwa tunacheza tena na ndio maana unawakuta wachezaji wapo chinio kidogo”.
Kwa matokeo hayo JKU imezidi kujiweka
kileleni wakiwa na alama 38, na Jang’ombe boys wakiwa nafasi ya 11 na 18.
No comments:
Post a Comment