Friday, 15 April 2016

Liverpool yaingia nusu fainali Europa League


Liverpool yatinga nusu fainali baada ya ya kushinda 4-3 dhidi ya Borrussia Dortmund

                  Hatua ya Robo fainali ya michuano ya Europa imeendelea tena Alhamisi kwa michezo minne, ambapo Liverpool imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 4 -3 dhidi ya Borrussia Dortmund.

Magoli ya Liverpool yamefungwa na wachezaji Divock Origi, Philippe Coutinho, Mamadou Sakho na Dejan Lovren.

Na magoli ya Dortmund yamefungwa na Henrikh Mkhitaryan, Pierre-Emerick Aubameyang na Marco Reus .

Sevilla imeiondoa Athletic Bilbao kwa changamoto ya penalti 5-4 kufuatia sare ya jumla ya 3-3 baada ya kila timu kushinda 2-1 mechi ya nyumbani.

Villarreal imeifunga Sparta Praga bao 4- 2 na Shakhtar Donetsk imeirarua Sporting Braga kwa mabao 4-0.

Kwa matokeo hayo Liverpool inaungana na Sevilla, Shakhtar Donetsk na Villarreal katika hatua ya nusu fainali.

No comments: