Atletico Madrid
yaicharaza Barcelona na kufuzu nusu fainali ya ligi kuu ya UEFA.
Mabingwa watetezi
Barcelona walifanya vyema katika mechi ya kwanza na kushindwa kuendeleza
msururu wao wa ushindi kwenye mechi ya marudiano.
Atletico Madrid
ilitembeza kichapo cha 2-0 kwa Barcelona na kuibandua kutoka kwenye
kinyang'anyiro hicho cha kuwania kombe la ligi kuu ya UEFA.
Magoli yote mawili ya
Atletico Madrid yalifungwa na mshambuliaji Antoine Griezmann katika dakika ya
36 na 88.
Baada ya matokeo hayo,
sasa Atletico Madrid itasubiria mpinzani wake wa nusu fainali atakayebainishwa
kwenye mchakato wa draw utakaofanyika siku ya Ijumaa.
No comments:
Post a Comment