Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Zanzibar
dhidi ya African Kivumbi timu ya Young Islander jana ilifuta makosa yake kwa
kuibamiza timu ya Madungu kwa jumla ya magoli 3-1 katika mchezo uliochezwa
kwenye uwanja wa Gombani.
Katika mchezo huo ambao watazamaji hawakuwa wengi Young
Islanders walianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 35 kupitia kwa
mchezaji wake Fahdi Ali, huku la pili likifingwa na Amour Issa kwenye dakika ya
44.
Na hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Young Islanders
walikuwa wanaongoza kwa magoli 2-0.
Kuanza kipindi cha pili Madungu walionekana kuja juu jambo
lililopelekea kujipatia bao kwenye dakika ya 55 lilifingwa na mchezaji wake
Kassim Juma ambaye aliingia akitokea benchi.
Dakika 2 kabla ya kumalizika kwa mchezo huo Fahdi Ali wa
Young Islanders aliiaandikia timu yake goli la 3.
Hadi dakika 90 za mwamuzi Hassan Gerei zinamalizika Young
Islanders 3 na Madungu 1.
Na katika mchezo mwenye wa ligi kuu ya Zanzibar Kanda ya
Pemba uliochezwa jana katika uwanja wa FFU Finya timu ya Shaba ya Kojani
imeendeleza ubabe kwa kuicharaza Okapi ya Msuka kwa jumla ya mabao 3-1.
Leo kutakuwa na michezo miwili, kwenye uwanja wa Gombani
Chipukizi wataikaribisha African Kivumbu na FFU Finya Mwenye watakuwa uso kwa
uso na Sharp Victor.
No comments:
Post a Comment