Kindumbwendumbwe cha ligi kuu ya Zanzibar kimeendelea tena
leo kwenye uwanja wa Gombani na FFU Finya majira ya alasiri.
Katika mchezo wa Gombani kati ya African Kivumb i ya Mwambe
na Chipukizi ya Chake Chake, A/Kivumbi imejikuta ikalala mbele ya wakongwe hao
kwa mabao 2-0.
Mchezo ulianza na kasi kwa temu zote kuonyesha umahiri wao wa
kupiga pasi maridadi, lakini hadi lakikaa 45 za kipindi cha kwanza kinakwisha
hakukuwa na mbabe aliyeweza kuziona nyavu za mwenzake.
Katika dakika ya 37 ya mchezo walimpumzisha Samir Ali Simai
na nafasi yake kuchukuliwa na Abdul-karim Ali, huku mwanzoni mwa kipindi cha
pili A/Kivumbi waliwatoa nje Fred Ramos na Ibrahim Abdalla na kuwaingiza
Zakaria Bakari na Ali Mussa.
Bao la kwanza la Chipukizi limefungwa na mchezaji Abdul-karim
Ali aliyetokea bench baada ya kuutumbukiza wavuni kwa urahisi mpira uliokoswa
na mlinzi wa A/Kivumbi Mustafa Moh`d katika dakika ya 65.
Alikuwa Abdul-Karim Ali kwa mara ya pili aliyewanyanyua
mashabiki wa Chipukizi kwa kuanzika bao safi katika dakika ya 88.
Na hadi mwisho wa mchezo huo Chipukizi 2 na African Kivumbi
hawakupata kitu.
Chipukizi tayari imeshashinda michezo yake yote mitatu
iliyocheza huku kwa A/Kivumbi akishinda mmoja,kutoka sare 1 na kufungwa mmoja.
Na huko kwenye uwanja wa FFU Finya Mwenge wakaisambaratisha
Sharp Victor kwa jumla ya magoli 2-0.
Kesho kutakuwa na michezo miwili pia,uwanja wa Gombani
Madungu watawakaribisha Aljazira na FFU Finya Okapi watavaana na Kizimbani.
No comments:
Post a Comment