Timu ya Strong fire imekubali sare ya mabao 2-2 walipocheza na White bird katika mchezo wa ligi daraja la kwanza taifa hatua ya sita bora kanda ya Unguja.
Mchezo huo uliosukumwa
ndani ya dimba la Amani majira ya saa kumi za jioni, Strong fire walianza
kuchezan vyema na ilipofika dakika ya 13 Ulimwengu Edi Mundi aliipatia Strong
fire bao la kuongoza.
Timu hizo ziliendeleza
kuonesha ushindani wa hali ya juu, na
Strong fire wakapata bao la pili lililofungwa na Hashim Ramadhan katika dakika
ya 34. Na timu hizo zilikwenda mapumziko Strong fire wakiwa mbele kwa mabao
2-0.
Katika kipindi cha pili
White bird walionekana kubadilika kwani walicheza mchezo kwa ajili ya kutaka
kuyarejesha mabao hayo, huku Strong fire walijisahau kabisa na kuridhika na
mabao mawili waliyoyapata.
Na ndipo Alphonce A.
Thomas akaanza kuipatia White bird bao la kwanza mnamo dakika ya 54, lakini pia
waliendeleza juhudi na kufanikiwa kusawazisha bao hilo baada ya Chande Abdalla
kufunga katika dakika ya 77.
Mtanange huo
ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
SALMA SPORT’S MEDIA
ilitaka kufahamu ni nini tatizo lililopelekea kwa timu ya Strong fire kurejeshewa mabao mawili katika kipindi cha
pili kocha Hassan Ramadhan amesema
kujiamini kwa wachezaji wake ndio sababu ya hayo yote.
“Tumeweza kucheza
vizuri kipindi cha mwanzo, kipindi cha pili walijiamini wameona mechi imekwisha
wenzetu wamefanya kazi wameweza kusawazisha magoli yote mawili, wachezaji wangu
walikuwa wanajiamini kwamba washapata magoli mawili na wakawa wanaamini time
yoyote watapata goli jengine lakini haikuwa hivyo”.
Aidha kocha wa timu ya
White bird Moh’d Abdul-kadir amesesma kuwa mchezo ulikuwa mgumu sana kiupande
wao hasa hasa kwa kipindi cha pili ndio maana wakasawazisha makosa na kuweza kufanikiwa kurejesha mabao mawili
katika kipindi cha pili.
“Mchezo ulikuwa mgumu
sana upande wetu sie kwa kipindi cha kwanza lakini baada ya kurudi niliweka vijana
wangu vizuri nimewaelekeza kwenye mchezo tumejipanga tumerejesha goli mbili”.
Matokeo hayo yameifanya
Strong fire kufikisha alama tano 5, na White bird kuwa na alama nne 4.
Kutokana na matokeo
yanavokwenda timu hizo bado hazijajihakikishia kupanda ligi kuu na kila timu imebakia
na mechi moja tu ili kujua kwamba wamepanda ligi kuu, hivyo ktokana na ligi
inavyokwenda timu hizi zitasubiri mchezo wao wa mwisho na hapo watawerza kujua
kama wamepanda au hawajapanda ligi kuu.
No comments:
Post a Comment