Kilabu ya Olympique Marseille inayocheza kwenye ligi kuu ya soka ya Ligue 1 nchini Ufaransa imemtimua kocha wake Michel.
Kilabu hiyo ilitoa
maelezo na kutangaza kumuondoa kocha Michel aliyekuwa ameletwa mwaka jana
kuziba pengo la kocha Marcelo Bielsa aliyejiuzulu.
Katika kipindi cha
miezi 8 ya ukufunzi wake, Michel ameweza kushinda mechi 8 pekee na timu ya
Olympique Marseille jambo ambalo ni kinyume na matarajio.
Maelezo zaidi yanaarifu
kwamba Olympique Marseille itaendelea kuwa chini ya kocha msaidiziFranck Passi
hadi mwishoni mwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment