Hatua ya sita bora ya ligi daraja la kwanza taifa kanda ya
Unguja leo imeendelea tena katika uwanja wa Amani kwa kuchezwa mchezo kati ya
timu ya Wakombozi wa ng’ambo Taifa ya Jang’ombe
walipopepetana na Chwaka.
Katika mtanange huo Taifa ya Jang’ombe wamekula sahani moja
na Chwaka baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Mchezo huo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani, Chwaka
walikuwa ndio wa mwanzo kuliona lango la Taifa kupitia mchezaji Kassim Khamis
katika dakika ya 19.
Mtanange huo ulikuwa wa kasi kwa kufanya mashambulizi kwa
kila upande na ndipo mchezaji wa Taifa Yussuf Mariano aliposawazisha katika dakika ya
44, na timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Na mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao
1-1.
Matokeo hayo yameifanya timu ya Taifa ya Jang’ombe kuwa nafasi
ya kwanza na alama nne (4) ambazo
sawasawa na timu ya Mundu, na Chwaka wao wapo nafasi ya tatu (3) na alama mbili
(2).
Katika michezo waliyokutana timu hizo katika mzunguko wa
kwanza na wa pili Chwaka walipoteza mechi zake zote dhidi ya Taifa, hivyo leo
imeonekana kuondoa uteja wao kwa kuwabana Taifa kwa kutoka sare ya bao 1-1.
No comments:
Post a Comment