Kocha Jose Mourinho
adaiwa kufanya mazungumzo na kilabu ya PSG nchini Ufaransa
Baada ya kimya kirefu
tangu kutimuliwa Chelsea, tetesi mpya zimeanza kuibuka kuhusiana na kocha Jose
Mourinho ambaye kwa sasa hana timu.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Uingereza, kocha Mourinho anadaiwa
kufanya mazungumzo na kilabu ya PSG nchini Ufaransa.
Katika siku za hivi
karibuni, Mourinho pia amekuwa akihusishwa na tetesi za uwezekano wa kupewa
fursa ya kuchukuwa nafasi ya Louis van Gaal na kuinoa Manchester United nchini
Uingereza.
Tangu mwaka 2013,
kilabu ya PSG imekuwa chini ya mkufunzi Laurent Blanc ambaye ameiwezesha
kunyakuwa mataji 9.
Mourinho mwenye umri wa
miaka 53 aliwahi kuwa mkufunzi wa Porto, Inter, Real Madrid na Chelsea.
Licha ya tetesi hizo
kugonga vichwa vya habari, kilabu ya PSG bado haijatoa maelezo yoyote kuhusiana
na madai hayo.
No comments:
Post a Comment