KAMPENI “FICHUA VIPAJI”
wambele mwenye mpira ni Braythoni Japheti
Mlinzi wa timu ya Simba “B”upande wa kushoto Braythoni Japheti ameamua kutoa mtazamo wake
kwa soka la Tanzania huku akijiuliza kwanini linashindwa kukua wakati vipaji
vipo vingi nchini.
Braythoni Japheti ameyasema hayo jana wakati alipokua
akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA juu
ya uwoni wake kwa soka nchini Tanzania.
Amesema “Ukiangalia vipaji Tanzania vipo vyakutosha ila ukuzaji
wa vipaji hivyo ndio imekua tatizo”alisema Braythoni Japheti
Amesema ukitazama vipaji vya vijana waliopo mitaani
utashangazwa kwanini nchi inashindwa kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya
soka, amesema kila kona watoto wacheza tena kwa viwango vizuri na vya
kuridhisha lakini hawana matunzo na ndio maana huishia mitaani tu.
Aidha amesema ni hali ya kusikitisha kwa wachezaji
wadogowadogo nishinda kupata usaidizi ili kukuza vipaji vyao “ Yani ukiwa na kipaji
itabidi ufanye jitihada zako mwenyewe ndio upate kuonekana la si hivyo itaishia
stori tu, sasa hapa ndio tunafanya nini”
Sambamba na hayo Japheti amesema “ Vituo vya ukuzaji vipaji nchini bado
havijawa vyakutosha kwasababu ukiangalia saivi ukiwa na kipaji bila kufika Dar basi wewe kiwango chako kitaishia vilabu vya chini
hutokuja kuonekana hata siku moja ”alisema
Japheti
Ametoa wito kwa viongozi kwa kusema kua wanatakiwa wawe makini kwa kuliona
hilo kwani vipaji vipo vya kila aina na nchini inaweza kupiga hatua kwa
wachezaji hao .
Amesema kuweka vituo vingi vya ukuzaji vipaji kila kona Ya T’z kutajenga hamasa na vijana
watacheza kwa moyo zaidi baadae mafanikio yanajitokeza yenyewe.
No comments:
Post a Comment