Sunday 3 April 2016

WALIOFANIKIWA KWA SOKA NCHINI NI KWA JUHUDI ZAO WENYEWE


Mlinzi wa timu ya  Ruvu Shooting  Hamis Seleman amesema  ni vizuri kwa wadau wa soka kufahamu kua mchezo huo nchini unaonekana kukua na kupandachati tofauti na kipindi cha nyuma.

Asema kukua huko si kwa kazi za viongozi au mamlaka ya michezo nchi  lakini ni kwa juhudi na bidii za wachezaji wenyewe wanazozifanya.

Seleman ametoa kauli hiyo jana alipokua akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA juu ya mtazamo wake katika soka la Tz.

Amesema ni dhahiri inaonekana kumekua na tofauti katika hali ya soka nyuma na kipindi hiki, imefikia hatua sasa mpaka nchi kutoa wachezaji wazuri wanaosifikana ndani na nje lakini yote hayo ni matunda ya nguvu zao wenyewe.

Aidha amesema ili kuzidi kuliinua soka nchini Tz ni lazima viongozi na wenye dhamana ya michezo wajidhatiti kwa nia njema ya kulikuza soka hapo kunaweza kufanikisha katika mafanikio zaidi.

Seleman amesema viongozi wa Tz hawawajibiki ipasavyo na ndio maana baada ya kupiga hatua mapema lakini imekua ni kurudi nyuma, ametolea mfano kwa kusema “viongozi hawa wala awachangii chochote kama wangekuwa wanamchango ile timu ya taifa ya Vijana ilioenda Brazil iko wapi sasa hivi”


Amemalizia kwa kutoa wito kwa wachezaji kuzidi kujikaza zaidi na kuweka malengo mbele hapo ndipo watakapofanikiwa na viongozi kwa upande wao watoe ushirikiana wa kutosha kwa wachezaji na kutafuta mbinu mbalimbali za kulikuza soka hapo ndipo nchi itakapo pata mafanikio zaidi.

No comments: