
Timu ya Bayern Munich yabeba taji la ligi ya Bundesliga kwa mara ya 4 mfululizo.
Bingwa wa taji la ligi
kuu ya soka ya Bundesliga nchini Ujerumani alibainika hapo jana baada ya mechi
za wiki ya 33 kuchezwa.
Mabingwa watetezi
Bayern Munich waliweza kuhifadhi taji lao kwa mara ya 4 mfululizo baada ya
ushindi wa 2-1 dhidi ya Ingolstadt kwenye mechi iliyochezwa hapo jana.
Bayern Munich
ilitawazwa bingwa wa taji la Bundesliga kwa kuwa ilitakiwa kupata ushindi ikiwa
imesalia wiki moja kabla ya ligi kumalizika.
Kwa mafanikio hayo,
Bayern Munich imeweza kunyakuwa taji lake la 26 la Bundesliga na kuendeleza
historia yake ya kuwa kilabu yenye mataji mengi zaidi Ujerumani.
No comments:
Post a Comment