
Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar JKU, leo imelala baada ya kufungwa goli 1-0 kutoka kwa Zimamoto katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa ndani ya uwanja wa Amani mjini Unguja.
JKU leo hawakuonesha
kabisa kiwango chao na wamecheza tofauti na walivyozoeleka, pia walikosa nafasi
za kufunga na kuwapa mwanya timu ya Zimamoto ambao walijipatia bao pekee.
Zimamoto wamepata bao
hilo kupitia mchezaji Amour Juma alilolifunga katika dakika ya 38.
JKU ni mchezo wake wa
tatu sasa kuupoteza katika mechi 20 walizocheza, tangu kuanza kwa ligi amabpo
wamepoteza walipokutana na Black sailor 1-0, pia wamepoteza kwa Miembeni 1-0,
na leo wamefungwa na Zimamoto 1-0.
Zimamoto sasa wamepanda hadi nafasi ya pili
wakiwa na alama 35 katika msimamo wa ligi hiyo,na JKU licha ya kuupoteza mchezo
huo lakini bado wanaongoza ligi wakiwa na alama 47.
No comments:
Post a Comment