Kiungo wa kati wa Ujerumani anayechezea kilabu ya Arsenal nchini Uingereza Mesut Özil, amezuru mji mtukufu wa Makkah nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza ibada ya umrah.
Mesut Özil ambaye siku
chache zilizopita alichaguliwa mchezaji bora wa Arsenal msimu huu, alisambaza
picha alizopiga Makkah kwenye akaunti yake ya mtandao wa jamii wa Twitter.
Maelfu ya mashabiki wa
Mesut Özil wanaomfuatilia kwenye mitandao ya jamii walivutiwa mno na picha hizo
alizosambaza mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid.
Kutokana na ustadi wake
aliouonyesha msimu huu na kilabu ya Arsenal, nyota huyo mwenye umri wa miaka 27
ameweza kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kwa ajili ya
kucheza kwenye mashindano ya EURO 2016 nchini Ufaransa.
No comments:
Post a Comment