Shirikisho la soka duniani Fifa limemtimua naibu katibu wake Markus Kattner kwa kujihusisha na ukiukwaji wa matumizi ya siri ya mamilioni ya dola.
Kattnet raia wa
Ujerumani mwenye umri wa miaka 45 alikua akiitumikia nafasi hiyo baada ya
aliyekua katibu Jerome Valcke kutimuliwa kazi kutokana na kashfa za rushwa.
Kufutwa kazi kwa
kiongozi huyu kulikuja mara moja baada ya bodi ya uchuguzi ya ndani ya Fifa
kugundua kulikua na ukiukwaji na uvunjaji wa majukumu yake.
Kulikuwa na ushahidi wa
kutosha kuonyesha mapungufu katika majukumu yake kwa kutumia pesa za ziada
ambazo waliamua kiasi gani rais, katibu mkuu na naibu katibu mkuu walipwe.
bbc.
No comments:
Post a Comment