Friday, 27 May 2016

MOURINHO ATHIBITISHWA MENEJA MPYA MANCHESTER UNITED


Mourinho

Jose Mourinho ametangazwa rasmi kuwa meneja mpya wa klabu ya Manchester United.

Ametia saini mkataba wa miaka mitatu.

Mreno huyo anachukua nafasi ya Mholanzi Louis van Van Gaal, aliyefutwa kazi Jumatatu siku mbili baada ya kushinda Kombe la Dunia.

"José kusema kweli ndiye meneja bora zaidi wa soka kwa sasa," naibu mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward amesema.

Mourinho, mwenye umri wa miaka 53, amesema: "Kuwa meneja wa Manchester United ni heshima kubwa sana katika mchezo huu. Ni klabu inayofahamika sana na kuenziwa kote duniani.”

Amesema amekuwa akihisi mvuto wa kutaka kuwa Old Trafford na kwamba daima amekuwa akisikizana na mashabiki wa United.

“Nasubiri kwa hamu kuwa meneja wao na kujivunia uungwaji mkono wao miaka ijayo.

“Kuna hisia fulani na upendo ambao huwezi kupata kutoka kwa klabu nyingine.”

Mourinho amekuwa bila kazi tangu  afutwe na klabu ya Chelsea Desemba mwaka jana.

Mourinho ametia saini mkataba baada ya  mazungumzo ya siku tatu baina yake, wakala wake Jorge Mendes na maafisa wakuu wa United.

Moja ya mambo ambayo anatarajiwa kuyafanya ni kumchukua mshambuliaji kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic, ambaye walifanya kazi pamoja wakiwa Inter Milan.


bbc.

No comments: