Uwanja ulikuwa na mashabiki 200 wakati wa mechi hiyo.
Klabu moja ya soka
nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi
mpya ya ufungaji mabao duniani.
Klabu hiyo ya Pelileo
Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika mechi ya ligi ya daraja
la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200.
Rais wa Indi Native
Diego Culequi amesema matokeo hayo hayakutarajiwa na wachezaji hawakuwa
wamezoea joto kali ambalo anasema lilichangia kushindwa kwao.
Mwandishi wa habari
Mwingereza Tim Vickery, ambaye amekuwa Brazil kwa miaka 20, amesema Bon Accord
kwa sasa wamejadiliwa sana katika vyombo vya habari Ecuador.
Mwenyekiti wa Arbroath
FC John Christison amesema ana wasiwasi kiasi kwamba rekodi yao waliyoiweka
1885 huenda ikavunjwa.
Amesema klabu hiyo
itasubiri uamuzi wa Guinness World Records.
bbc.
No comments:
Post a Comment