Chama cha mpira wa miguu nchini Zanzibar ZFA kimeshauriwa
kupanua wigo katika kukuza soka nchini ikiwamo kua na muono wa mbali katika
kutafuta wachezaji vipaji badala ya kutazama haokwa hao kila siku.
Imesemwa kua tatizo kubwa linaloikabili Zanzibar kutoendelea
kisoka ni wadau kunga'ng'ania wachezaji kutazama pamoja tu kila siku wakati
kuna wachezaji wazuri na wenye vipaji vijijini lakini wanashindwa kuonekana
kutokana na kutokua na watu wa kuonesha.
Haya yamesemwa na mmoja kati ya wadau wa soka nchini
anaecheza kabumbu binafsi katika safu wa ushambuliaji(hakujiunga na timu) Khali
Ali Sabary jana alipokua akizungumza na SALMA SPORT'S MEDIA katika kiwanja cha
Kianga juu mtazamo wake katika maendeleo ya soka la Zenji.
Alisema"huu mchezo wa mpira sasa nchini umekua ni balaa
wachezaji wapo tele tena ukiwaona unaweza kujiuliza ni kwanini tunashindwa
kuendelea na vipaji ndio kama hivi,lakini wapi imekua hawaonekani hata siku
moja mwishowe hukatika tamaa na kuamua kufanya mambo mengine."alisema Sabary.
Alipolulizwa na mwandishi wa habari hizi juu ya nini
kifanyike kiufundi ili kuipa hadhi nchi kisoka Sabary amejibu kua ni nyema ZFA
ikazingatia vijana wadogowadogo kwani wana uwezo wa kutosha na wakiwezeshwa
wanaweza kuliletea sifa taifa halikhalika kufungua vyuo vya soka kama ilivyo
kwa nchi nyengine hapo ndipo Zanzibar itakapotajika kitaifa na kimataifa.
Amemalizia na wito kwa vijana kutovunjika moyo mapema bali
waendelee na mazoze kama kawaida huku wakitanguliza malengo mbele akisema ndiko
kutakapowafikisha mwisho wa safari yao ya matumaini na mafanikio.
SALMA SPORT'S MEDIA ilishuhudia uwezo wa mchezaji huyu Rajabu
(SABARY)na kuridhishwa na kiwango chake laiti kama wadau wa soka wanamuona huyu
tunaamini mazuri yaanweza kutokezea na wapo wengi kama hawa
No comments:
Post a Comment