Mwanariadha Nesta Carter wa timu ya Jamaica ya mbio za
kupokezana vijiti inayomjumuisha Usain Bolt anadaiwa kutumia dawa za kusisimua
misuli baada ya kufanyiwa ukaguzi.
Nesta ambaye alishinda medali ya dhahabu pamoja na Bolt kwenye
mashindano ya mbio za 4x100m za kupokezana vijiti kwenye olimpiki ya Beijing
mwaka 2008 alifanyiwa ukaguzi na kugundulika kutumia dawa za kusisimua misuli.
Endapo Nesta atathibitishwa kutumia dawa za kusisimua misuli
kwenye ukaguzi wa mwisho utakaofanyika, basi atawaweka wenzake matatani.
Hatua hiyo huenda ikasababisha Bolt kuvuliwa medali ya
dhahabu moja aliyoshinda kwenye mbio hizo za 4x100m.
No comments:
Post a Comment