Serikali na wadau wa michezo nchini Tanzania hasa Zanzibar
wametakiwa kutolalia upande mmoja tu kunua na kuendeleza kwa kasi michezo na
badala yake wameshauriwa kuangalia kila kona ya michezo inayochezwa nchini.
Kauli hiyo imetolea
leo hii na mchezaji wa mchezo wa karati Hashim Mohammed maarufu Fund Hashim
wakati alipokua akizungumza na mwanamichezo wako Salma Hassan mjini Zanzibar.
Amesema mchezo wa
karati ni mchezo muhimu sana katika nchi na ni mchezo unaopendwa sana na
unamashabiki wengi lakini umekua ni tofauti kimuonekana na michezo mengine kama
mpira wa miguu nchini Zanzibar.
Fund Hashim amesema yeye anauthamini sana mchezo huo kwakua
ni mzuri katika kujenga afya ya kiwiliwili na saikolojia ya akili na maetoa
wito kwa vijana nchini kujiunga na mchezo huo ili kujiweka sawa katika hali ya
ulinzi na kiusalma.
Akijibu suala la
mwanamichezo huyo kuhusu malengo yake juu ya mchezo huo amesema amesema
"malengo yangu nikufiki katika kiwango cha juu na hatimae nishiriki katika
mashindano ambayo yataniletea sifa mimi mwenyewe na kuliwakilisha vyema taifa
langu ndani na nje ya nchi kwani uwezo ninao na nazidi kujiweka sawa"
Akizidi kuelezea
malengo yake amesema kubwa zaidi anatarajia kupokea mafunzo vizuri kutoka kwa
walimu wake ili baadae aweze kuwa mwalimu mzuri kwa wanafunzi katika siku za
usoni.
Aidha amezungumzia
changamoto iliyopo mbele yake ambapo amesema pasingekuwepo na uchaguzi wa
marejeo basi muda huu angekua ameshavaa mkanda wa “Green Orange” kwani alikua
yupo katika mtihani ili kuvishwa mkanda huo lakini kutokana na kuwepo uchaguzi
chuo hicho kufungwa na kubakia na kiwango cha shot kan karate.
Fund Hashim ni
mchezaji mzuri wa karati na anauwezo mzuri katika upiganaji huo,anajifunza
kupitia chuo cha Amani Moden Kar
No comments:
Post a Comment