Mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania unaonekana kua na
changamoto nyingi zinazopelekea kutokukua kwa viwango vya juu kwa timu
mbalimbali hapa nchini.
Hayo yamesemwa na mmoja miongoni mwa dawau wa soka nchini
Ahmad Ali Bakar kutoka Dar es Salam alipotoa maoni yake juu ya soka la Tz kwa
mwanamichezo wako Salma Hassan.
Amesema hali hiyo inasababishwa na baadhi ya viongozi
kutokua na umakini na kazi zao lakini pia baadhi ya timu kubwa kutojali na
kuthamini vipaji vya wachezaji akisema kua wakikuona unafaa na kiwango chako
kipo vizuri wanakuchukua ila ukichuja tu kidogo basi huna tena thamani katika
timu hiyo amesema huko ni kupoteza vipaji.
Amemalizia kwa kutoa ushauri wake kwa viongozi wa soka
nchini kuwa wafanye kazi za ufundishaji kwa umakini na kuweka upande maslahi
yao binasi.
No comments:
Post a Comment