Saturday, 27 February 2016

ILI SOKA LIKUE NCHINI TIMU KUBWA ZIMILIKI VIWANJA VYAKE WENYEWE.


Mashabiki na wadau wa soka nchini wamesema kua soka la Tanzania bado lipo katika kiwango cha chini na si cha kurisha kutokana na mfumo mbaya wa uwendeshaji wa soka hilo.

Wamesema kua ukiachana na viongozi , timu zenyewe zimekosa misingi bora ya kuibua vipaji vyao wenyewe kutokana na utaratibu wa kufikiria kwa upana juu ya ukuzaji wa soka kutokuwepo.
Mmoja miongoni mwa wadau hao Najeli Kihongosi kutoka Iringa aliezungumza na SALMA SPORT’S MEDIA juu ya mtazamo wake katika soka la Tanzania.

Kihongosi amekiri kwa kusema  ni kweli soka la hapa nchini ni chini ya kiwango na itachukua muda kukua, ametolea mfano kwa kusema  vilabu vingi hapa nchini havina Academy za kukuza vipaji ,hawana  viwanja vyao wenyewe lakini pia uongozi wa TFF haujasimamia uanzishwaji wa Academy kwa kila kilabu.

Amesema kama TFF wangeweza kusimamia hili la uwanzishwaji wa Academy basi nchi ingekua na kutajika pakubwa kwa soka.

Aidha amesema changamoto nyingine ni uchumi hafifu kwa vilabu vingi hapa nchini kiasi ambacho wanashindwa kuyafikia malengo yao waliojipangia kutokana na kua na uchumi mdogo.

Kwa upande mwengine Kihongosi ametoa wito kwa wadau na wanasoka nchini kwa kusema, timu kubwa na kongwe kama Simba na Yanga na nyenginezo ni lazima wawe na viwanja vyao kwani wana rasilimali watu wengi kuzisaidia timu zao.

Pia amesema, timu za mikoani zitafute udhamin ili wajengewe viwanja na wadhamini nao pia wajitokeze kudhamini timu hizo kwani zitakapoweza kua na Academy hizo zitazalisha vipaji vya hali ya juu.


Halkadhalika ameitaka TFF ihakikishe inasimamia sheria za mapato ili kuwa na uchumi imara huku  ikihakikisha  mianya yote ya uchakachuaji wa ticket unakomeshwa pia itafute udhamin imara ili timu ziwe 20 ligi kuu na kuboresha ratiba kuepusha upangaji matokeo na kupata kilichobora.