Wadau wa soka nchini wameonesha kukasirishwa na tabia ya
baadhi ya wachezaji wengi kwa upande wa Zanzibar kwa tabia ya kucheza soka kama
ni mazoea tu au burudani ya kawaida pasipo na kuutilia nguvu, hali ambayo
imedaiwa kuwa ndio sababu moja wapo ya timu za Zanzibar kutofanya vizuri katika
mashindano tofauti.
Mmoja miongoni mwa wadau wa michezo kutoka Tanzania bara
Bw:Abdul Jimbo pia amelizungumzia soka la Zanzibar na wachezaji wake kwamba bado wanachukulia
mpira kama ni kitu cha kawaida wakati wenziwao wa Tanzania bara wanachukulia
kama ni sehemu ya ajira na ndio maana hujituma kwa bidii na wanaonekana wapo
juu zaidi ya visiwani.
“Zanzibar kuna vipaji vingi sana na kuna watu kama wataamua
kweli basi soka litachezwa lakini tofauti ya Zanzibar na Bara ni moja tu, wachezaji wengi wa
Zenji wanafanya mpira kama sehemu ya
kupata burudani tu ila wenziwao wa Bara wachezaji wanafanya mpira kama ajira
yao ndio maana utaona soka la Bara kwa upande Fulani hivi lipo juu tofauti na
Zenji”alisema Jimbo.
Jimbo amesema ni lazima wachezaji wa Zanzibar sasa wabadilike
na kutilia mkazo zaidi mchezo wa soka akisema duania ya sasa, soka ni ajira na
inayolipa ikiwa utafanya kazi nzuri.
Kwa uapnde mwengine
ameshauri mamlaka za soka nchini kuzidisha vyuo vya mpira kua wingi na
ufundishaji uwe wa kuwafanya watoto waone mpira ni kama sehemu ya maisha yao
hivyo kutainua viwango vya soka na hatimae taifa litasifika kama yalivyomataifa
mengine.
Ametolea mfano wa taifa la Brazili akisema mpira ni moja ya utamaduni wao, hivyo mtoto
tokea anakua anafahamu kama soka ni sehemu ya ajira.
Pia amesema walimu wa soka
wawafunze wachezaji wao jinsi ya kucheza mpira wa ushindani na sio mpira
wa burudani tu.
No comments:
Post a Comment