Wednesday, 2 March 2016

JECHA KUANZA MAZOEZI RASMI KESHO




Kiungo Mshambuliaji wa Kijichi Ali Jecha “Vigema” kesho anatarajiwa kurejea mazoezini katika klabu yake ambapo alikaa majeruhi kwa kipindi kirefu.

Jecha amewaahidi mashabiki wake wategemee makubwa kutoka kwake ambapo anataka kuisaidia timu yake ya Kijichi kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja.

“ Hali yangu ya afya sasaivi ipo vizuri na kesho naanza mazoezi katika timu yangu ya Kijichi, wapenzi wangu na wa Kijichi wote waniunge mkono naamini ntakuwa vizuri na ntawafurahisha”. Alisema Ali (Alcantara)

Kwasasa Ali Vigema anakipiga timu ya Kijichi kwenye ligi kuu soka Zanzibar Kanda ya Unguja na hakuwahi kucheza hata mchezo mmoja kwenye ligi hiyo kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Mchezaji huyo anauwezo binafsi wa kumiliki mpira na kuudhibiti bila ya adui kumpokonya, pia ana uwezo mkubwa kupiga chenga na kupiga mashuti makali langoni mwa wapinzani.


Jecha pia aliwahi kuchezea timu ya Kilimani city, Maji maji, Magomeni na alipokuwa mdogo kwenye ligi za Central Wilaya ya Mjini alikipiga kwenye timu ya Javerlion, Aston Villa, FC Ajax ya Bakari Rais, Leeds United ya Babu Khatib na FC Natural na alikuwa anaogopewa sana na timu pinzani kutokana na uwezo wake binafsi.

No comments: