Walimu wa soka nchini (makocha) wametakiwa kujitofautisha na
wanasiasa na badala yake wafanye kazi za kiuwalimu ili kutoa vipaji vya uhakika
nchini ili baadae kuliletea sifa taifa.
Wito huo umetolewa na mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa
timu ya “Magirisi” daraja la pili na mdau wa michezo leo hii Bwnana Maulid Ali (MAJIN) wa Meli nne Zanzibar wakati alipokua akizungumza na mwanahabari wako Salma Hassan juu ya maendeleo ya soka la
Zenji.
Amesema soka la zenji linashindwa kukua kwa sababu baadhi ya
walimu wamekua hawana tofauti na
wanasiasa kwa kile alichokiita porojo jingi.
Majin amesema walimu hao wamekua ni wakuropokwa ovyo kwa
maneno mengi pasipona ufundishwaji mzuri hatime timu zinadumaa na kila siku zinakua katika
kiwango kile kile.
“soka la zenji kwa sasa
ni tofauti sana zamani kwa sababu viongozi wanaoongoza soka siku hizi sawasawa
na wanasiasa hawana zaidi ya kuporoja kwingi”alisema Majin.
Akijibu suali la mwandishi wa habari hizi kwanini kumekua na
tabia ya kununua wachezaji kutoka nje ya nchi wakati inasemwa kuwa nchini mwetu
kuna vipaji lakini havithaminiwi amesema “Kwanza wachezaji wetu wa ndani hasa
hapa zenji wanachukulia mpira ni kama starehe lakini kwa wenzetu mtu ni kama
ajira yake, ninachotaka kuwambia waufanye huu mpira ni kama ajira,kwa hilo tu nahakikisha tutafika mbali”
Pia amotoa wito kwa viongozi ambao hawana utashi wa mpira
waache kushuhulikia kazi hiyo kwasababu
ni moja kati ya pingamizi za timu kutoshafanya vizuri na badala yake kuwe na na viongozi wanaojua nini maana ya soka, hapo Zanzibar
itainuka na kutajika.
No comments:
Post a Comment