Thursday 10 March 2016

MRISHO NGASA BADO KUNG’AA


Mchezaji wa Free State Stars ya Afrika Kusini raia wa Tanzania Mrisho Ngassa bado rikodi yake ya soka haijawaridhisha mashabiki wengi wa soka duniani.Kwa harakaharaka waweza kufikiria kwamba bado hajakua kiuchezaji kutokana na kutoonekana kinara wa magoli au usababishi wa magoli.

Habari zinasema Takwimu zake siyo nzuri sana klabuni hapo. Hii imetokana na pale baada ya kucheza mechi zisizopungua kumi na tano(15)  bila ya mafanikio ya kuingiza bao hata moja tokea ajiunge na klabu hiyo mwishoni mwa mwaka jana.

Ingawa mashabiki baadhi yao wanamatumaini na mshambuliaji huyo huku nae kadiri ya siku zinavyosonga anaonekana akijpa moyo katika uchezaji wake.

Baada ya kuongea na wadau mbalimbali wa soka wengi miongoni mwao wadai pengine Ugumu wa PSL yawekezana kuwa ni chanzo cha kutofunga akiwa na Free State hadi sasa takribani timu zipo kwenye raundi ya 21 ya ligi huku mfungaji anayeongoza kwa ufungaji raia wa Zambia, Collins Mbesuma amefunga goli 12 kwenye klabu yake ya Mpumalanga Black Aces.


Andrea Filleicia raia wa Ubeligiji  wa timu ya Free State mchezaji mpaka sasa yeye ndio aliyefunga magoli mengi na mpaka sasa ameshafunga magoli sita.  

No comments: