Katika kuelekea hatua ya nane bora kwa upande wa mpira wa
miguu wilaya ya Magharibi, jana viongozi wa ZFA Wilaya ya Magharib walifanya
kikao kilichowakutanisha Makatibu wa timu zilizotinga hatua hiyo.
Kikao hicho kilifnyika katika ofisi za ZFA wilaya ya
Magharibi huko Mwanakwerekwe Zanzibar, na viongozi hao waliweza kuzungumzia
mambo mbalimbali kuhusu hatua hiyo.
Mara baada ya kujadili mambo hayo SALMA SPORT’S MEDIA ilitaka
kufahamu wamekubaliana vipi kuhusu hatua hiyo? Katibu wa ZFA Wilaya ya Magharibi Omar Abuu amesema
kwamba.
“ligi itaanza siku ya Jumatano muda wowote kwa mujibu
tulivukubaliana, kuhusu viwanja vilabu vingi vimeomba tutumie wiwanja vilevile
tulivyokuwa tunatumia mwanzo pia tumezungumza kuhusu muda wa kuanza mechi,
vilabu vifike mapema uwanjani ili dakika 90 zipatikane kwa muda wote wa
mchezo”.
Aidha amezungumzia kuhusiana na mikakati yao amesema “mikakati
yetu ni kua tunajua kama baadhi ya viwanja vingi havina alama lakini tutajitahidi
kabla ya kuanza mechi hii ya nane bora turejeshe zile alama zilizopotea kwa
mvua”. Aliongeza Omar.
Hivyo amewataka mashabiki waende kushangiria na wala wasiende
na vurugu yoyote ile ili mpira uzidi kukua katika wilaya ya Magharibi.
Timu zilizotinga hatua ya nane bora ni:
Bambuu.
Beach Boys.
Chukwani.
Kisauni.
Mfenesini.
Nyangobo.
Villa.
Zantex.
No comments:
Post a Comment