Nyota wa zamani wa Uingereza David Beckham, anaarifiwa kununua ardhi nchini Marekani kwa ajili ya ujenziwa uwanja wa soka wa timu yake anayoimiliki.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na timu hiyo ya Miami Beckham United, iliarifiwa kwamba mmiliki huyo amenunua ardhi ya uwanja katika eneo la Overtown lililoko mjini Miami.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba ujenzi wa uwanja wa soka utaanza rasmi baada ya idhini kutoka kwa idara husika mjini humo.
Timu ya Miami Beckham United inatarajiwa kushiriki kwenye ligi kuu ya soka ya Marekani ya MLS mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment