Timu ya
Raskazone jana imetoka sare ya bila kufungana walipocheza na Negro katika
mchezo wa ligi daraja la pili wilaya ya Mjini uliosukumwa ndani ya dimba la
Amani.
Katika mtanange
huo timu hizo zilionesha upinzani wa hali ya juu kwa kila timu kutaka kuondoka
na ushindi, kwani zilipata nafasi nyingi za kufunga lakini umaliziaji ulikuwa
ni mbovu kwa timu zote hizo.
Na mchezo
huo ulimalizika kwa kutoka suluhu ya bila kufungana.
Akizungumza na
SALMA SPORT MEDIA, kocha wa Raskazone Moh’d Shubeir (Babu shube) amesesma kuwa
timu bado ni mpya na anahitaji kuitengeneza.
“Timu bado
mpya natengeza na ina matatizo mengi unajua mpira tofauti na lai kwenye friji asubuhi utaweka maji jioni
utapata barafu huu mpira una mambo mengi, una mapungufu megi na ndio maana
unachezwa katika sehemu ya wazi lakini bado najipanga kutengeza timu”.alisema
kocha Shube.
Pia aliendelea
kusema, “nilishasema na naendelea kusema nahitaji point tatu tu ili nibakishe
timu katika daraja nimebakisha mechi tatu nahitaji point mbili inshaallah kwa
uwezo wa mungu nitapata iyo nafasi na nitaibakisha hii timu mwakani
nitatengeneza”.
Aidha kocha wa timu ya Negro Hassan Abdul-Rahman
Saidi amesema kuwa mechi ilikuwa ni nzuri,
“Mechi ilikuwa
nzuri lakini nafasi tumezipoteza nyingi kiukweli ilikuwa si bahati yangu lakini
nafasi tumezipoteza nyingi kwani wanapoingia katika maeneo ya umakini wanakuwa
na presha na ndio wachezaji wetu wengi wa hapa Zanzibar,madhali nina muda wa
kuiandaa timu vizuri hapa kwa sabau nimepewa siku kama nne saivi timu hii
nategemea kwamba yatakuwa mambo mazuri kwa sababu nitafanyia mazoezi ya
umaliziaji na muda mwingi tutafanya mazoezi ya umaliziaji”. Alisema kocha
Hassan.
No comments:
Post a Comment