Salma Sport's Media

Sunday, 13 March 2016

SASA MAMBO SAWA PEMBA


Posted by Unknown at 07:53:00
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

TANGAZO

TANGAZO
Tumia fursa hii kwa kutuletea tangazo lako.

ZILIZOSOMWA KWA WINGI WIKI HII

  • WAAMUZI WA SOKA NCHINI NDIO KIZINGITI KWA SOKA LA TZ
  • Jee unamjua Johan Cruyff ? kawaida ya alikuwa akivaa jezi namba 14 unajua ni kwanini.soma hapa.
  • WACHEZAJI WAPO WENGI NI KWANINI ZENJ TUNAGANDA JIBU HILI HAPA.
  • Ghana kuandaa mashindano ya Marathon kwa ajili ya amani
  • JKU WAZIDI KUJIWEKA KILELENI HUKU POLISI WAKIWA KATIKA WAKATI MGUMU.NA PEMBA NAKO KAMA KAWA.
  • BASKETBALL INAWEZA KUIPASIFA ZANZIBAR
  • HATA KABLA YA GOLI LAKE DHIDI YA AZAM TAYARI JUMA ABDUL AMETHIBITISHA YEYE NI BORA
  • STRONG FIRE YALALA 2-1 KUTOKA KWA MUNDU.
  • MAN UTD YATINGA ROBO FAINALI FA CUP, GOLI LA MATA NDIYO HABARI YA MJINI
  • MESUT ÖZIL AZURU MAKKAH KWA AJILI YA KUTEKELEZA IBADA YA UMRAH

HABARI MPYA

Loading...

HABARI ZA KITAIFA ZA KINA TEMBELEA HAPA

HABARI ZA KITAIFA ZA KINA TEMBELEA HAPA

HABARI ZA KIMATAIFA ZA KUVUTIA

HABARI ZA KIMATAIFA ZA KUVUTIA

TEMBELEA KUJUA KILICHOJIRI

TEMBELEA KUJUA KILICHOJIRI

NI MCHANGANYIKO WA HABARI.

NI MCHANGANYIKO WA HABARI.

NI UKURASA BORA KWAKO

NI UKURASA BORA KWAKO

About Me + Maelezo

About Me + Maelezo
Blog hii imeanzishwa nchini Zanzibar na inaendeleza kazi zake Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, Inatumia lugha ya kiswahili na kingereza kwa uchache ili kuhabarisha kuhusu maswala mbalimbali ya kimichezo ndani na nje ya Tanzania. Salma Hassan ni mwandishi wa Habari za Michezo.Uzoefu wangu ni miaka mitatu na nimehitimu katika chuo cha Uwandhishi wa Habari Zanzibar (ZJMMC) katika ngazi ya Stashahada,kwa habari,taarifa au tangazo wasiliana nami kupitia +255779518500 / salmahassan040@gmail.com Ahsante

TAFUTA HABARI

Salma Sport's Media

WATEMBELEAJI.

page visitor counter
who is online counter blog counter

who is online counter blog counter

WATEMBEAJI NA BENDERA

HII NI SEHEMU MAALUM KWA WASOMAJI WETU WA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA MAGAZETINI NDANI NA NJE YA NCHI

HII NI SEHEMU MAALUM KWA WASOMAJI WETU WA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA MAGAZETINI NDANI NA NJE YA NCHI

MAGAZETI 05.06.2016 Wawili waenguliwa uchaguzi Yanga

WANACHAMA wawili kati ya 20 wameenguliwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uongozi ndani ya Klabu ya Yanga katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Juni 11 mwaka huu.

Mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya Yanga, Bakili Makele alisema jana kuwa wanachama hao wameenguliwa kutokana na kushindwa kuwasilisha vyeti vyao vya shule. Waliondolewa kwenye mchakato huo ni Yusuf Mahandeni na Leonard Marango.

Alisema wajumbe wengine wote wamepitishwa na leo kuanzia asubuhi hadi saa saba mchana utafanyika usaili kwa wagombea wote na wametakiwa kuwasili na vyeti vyao halisi vya kidato cha nne na kadi za uanachama.

“Pia kuanzia kesho (leo) saa saba tutaanza kupokea mapingamizi kwa wagombea waliopitishwa kama yatakuwepo na majina yatabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa klabu,”alisema.

Mpaka jana, uchukuaji fomu ukifungwa nafasi ya Mwenyekiti aliyechukua fomu ni Yusuf Manji pekee akitetea nafasi yake, na kwa upande wa Makamu Mwenyekiti ni Clement Sanga.

Wajumbe ni Samweli Lukumay, Salum Mkemi, Beda Tindwa, David Ruhago, Lameck Nyambaya, Ayub Nyenzi, George Manyama, Sylvester Haule, Siza Lyimo, Hussein David, Hashim Abdallah, Athuman Kihamia, Pascal Laizer, Godfrey Mheluko, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Mchafu Chakoma na Tobias Lingalangala.

Wakati mambo yakiwa hivyo Yanga, kwa upande wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), fomu zimeendelea kudoda huku Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo ikitarajiwa kukaa leo huku ile ya maadili ikikaa kesho kabla ya kutoa maamuzi yake juu ya uchaguzi huo wa klabu hiyo ya Jangwani.

Tayari Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Aloyce Komba amejiuzulu kusimamia uchaguzi huo kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili alizotuhumiwa na Mwenyekiti wa Yanga, kuwa anapanga hila kumuondoa ndani ya klabu hiyo kwa kosa la maadili kwa kile kinachodaiwa kusigina katiba ya klabu hiyo.

Kwa upande wa serikali (BMT) na TFF bado inatambua uchaguzi halali wa Yanga ni ule wa Juni 25 mwaka huu na sasa utasimamiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya TFF, Domina Mideli.

credit by habarileo.

MAGAZETI 05.06.2016 Stars fungu la kukosa

TAIFA Stars imeaga rasmi katika mbio za kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon), itakayofanyika mwakani nchini Gabon.

Safari ya Stars ilihitimishwa jana, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Misri kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa kundi G.

Matokeo hayo yanawafanya Misri wamalize mechi za Kundi G wakiwa na pointi 10 baada ya mechi nne, wakishinda tatu na kutoka sare moja, wakati Tanzania inabaki na pointi yake moja na inashika mkia nyuma ya Nigeria yenye pointi mbili.

Stars ilikuwa na kibarua kigumu, kwani ilikuwa inatakiwa kushinda mabao zaidi ya 3-0 dhidi ya Mafarao hao ili iweze kufuzu kwa michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Misri uliopigwa jijini Alexandria, Stars ilifungwa mabao 3-0 na baada ya kujitoa kwa Chad katika kundi hilo la G, Stars ilikuwa na karata moja ya kutakiwa kuifunga Misri ili iweze kufufua matumaini ya kufuzu kwa michuano hiyo.

Katika mchezo wa jana, Stars walianza kwa kasi wakitawala katika dakika 20 za mwanzo, lakini kutokana na umakini wao mdogo wakashindwa kupenya safu ya ulinzi ya Misri.

Misri walianza kuhesabu bao la kwanza katika dakika ya 43 lililofungwa na Mohamed Salah, baada ya kupiga mpira wa faulo iliyosababishwa na Haji Mwinyi na shuti lake lilikwenda moja kwa moja wavuni. Kipindi cha pili kilianza kwa Misri kufanya mabadiliko kwa kumtoa Mohamed Ibrahim na kumuingiza Amr Mohsen.

Nahodha wa Stars, Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika Klabu ya Genk, alikosa penalti katika dakika ya 53 baada ya Himid Mao kuchezewa rafu ndani ya eneo la hatari na Mohsen.

Misri ilipata bao lake la pili katika dakika ya 58, mfungaji akiwa ni yule yule, Salah ambaye anaichezea Klabu ya AS Roma ya Italia, baada ya kumzidi mbio beki Aggrey Moris.

Stars, licha ya kufanya mabadiliko katika dakika ya 61 kwa kumuingiza John Bocco ambaye alichukua nafasi ya Elias Maguli, lakini hadi kipenga cha mwisho kinalia hawakuweza kupenya ngome ya Misiri na matokeo kubakiwa kuwa 2-0.

Stars: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali/Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dk68, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Himid Mao, Thomas Ulimwengu/ Deus Kaseke dk73, Mwinyi Kazimoto, Elias Maguli/John Bocco dk62, Mbwana Samatta na Farid Mussa.

Misri: Essam Kamal Tawfik, Alg Gabr Mossad, Ramy Hisham Abdel, Mohamed Abdel Sayed, Abood Abdulrahamn Amed, Tarek Hamad Hamed, Mohamed Nasser Elsayed, Mohamem Ahmed Ibrahim, Abdallah Mahamoud Said na Nagram Mohsin Fahmy.

credit by habarileo

MAGAZETI 05.06.2016 Gavana kufunga bonanza la michezo na BoT

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Benno Ndulu atafunga bonaza la siku mbili la kuadhimisha miaka 50 ya BOT tangu kuanzishwa kwake.

Bonaza hilo lililoanza jana, linafikia kilele leo kwenye Uwanja wa Sigara jijini Dar es Salaam, likihusisha Wizara na Taasisi mbalimbali za kifedha, ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), CRDB, NMB, PSPF, Wizara ya Fedha na BoT wenyewe.

Michezo inayoshindaniwa ni mpira wa kikapu, soka, kuvuta kamba na netiboli ambapo kwa upande wa Wizara ya Fedha iliibuka kidedea jana katika mpira wa netiboli, baada ya kuinyuka PSPF na TRA na kukata tiketi ya kutinga fainali leo ambapo itamenyana na BoT, mchezo utakaofanyika asubuhi.

TRA itamenyana na Benki ya Barclays katika fainali ya mpira wa kikapu. Katika mchezo uliofanyika jana, TRA walionesha ubabe baada ya kuibugiza PSPF magoli 22 -16, na baadae ikainyuka Barclays magoli 19-15 na kufanikiwa kutinga fainali. Barclays wamefanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kuinyuka Wizara ya Fedha na Mipango magoli 32-5.

Kwa upande wa mpira wa miguu, Benki ya NMB iliinyanyasa CRDB kwa kuwachapa mabao 3-0, Barclays ikaonesha ubabe kwa kuinyuka TRA mabao 4-0. Kwa upande wa kuvuta kamba, Hazina waliibuka kidedea baada ya kuwabwaga TRA, hivyo kutinga hatua ya fainali ambapo leo watamenyana na BoT.

credit by habari leo.

http://salmasportmedia.blogspot.com/. Awesome Inc. theme. Powered by Blogger.