Tuesday 15 March 2016

USIKUBALI KUHADITHIWA LIGI KUU YA ZANIBAR KANDA YA UNGUJA LEO HII, JE! POLISI WATAONDOKA MKIANI?


Baada ya mapumziko ya siku kadhaa ya ligi kuu Zanzibar kanda ya Unguja, itaendelea tena leo hii ndani ya dimba la Amani majira ya saa kumi za jioni.

Katika mtanange huo utazikutanisha timu ya Polisi na Kimbunga, huku kila timu ikwa inataka ushindi katika mechi hiyo.

Polisi wakiwa bado hali ni tete, wataingia uwanjani wakiwa nafasi ya mwisho na alama zao ni nane (8), huku wakiwa wamepata ushindi mechi moja tu katika michezo kumi na nne (14) waliyocheza.

Polisi watahitaji ushindi katika mchezo wa leo ili waondoke mkiani na nafasi hiyo wawaachie timu ya Mtende ambayo wana alama tisa (9) wamewazidi kwa alama moja timu ya Polisi.

Kwa upande wa Kimbunga wataingia dimbani wakiwa wamecheza michezo kumi na tano (15) wameshinda mechi sita (6), wa wapi nafasi ya kumi (10) na wana  alama 20.

Kimbunga wana nafasi nzuri ya kupata ushindi kutokana na kufanya vyema mechi zake zilizopita, ukilinganisha na Polisi ambao wanaonekana kudorora kwa mechi zao.

No comments: