Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) leo imeaga
rasmi mashindano ya kombe shirikisho barani Afrika baada ya kupokea kichapo cha
bao 1-0 kutoka kwa SC Villa ya nchini Uganda.
JKU imepokea kichapo hicho wakiwa katika uwanja wao wa
nyumbani wa Amani, baada ya mchezaji wa SC Villa Ambroso Kirya kuweka kambani
bao katika dakika ya 45 kuanza tu kwa kipindi cha pili.
Katika mtanange huo JKU walianza kucheza vizuri katika
kipindi cha mwanzo na waliutawala mpira takriban dakika zote za kipindi hicho
katika kipindi cha mwanzo JKU walipata nafasi nyingi na walikosa mabao ya wazi.
Kocha mkuu wa JKU Malale Hamsini Keya wakati alipokuwa
akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA, amesema kwamba mechi ya leo imejirejea
kutokana na kucheza kama walivocheza kule Uganda lakini wachezaji wake pia
wamemuangusha zaidi.
“Game ya leo imejirejea zaidi kwa sababu hata ile ya Uganda
vile vile tulicheza vizuri kama hivi lakini tatizo kubwa nafasi nyingi
tunazitengeza lakini hatuzitumii vizuri bila shaka leo tumeliona lakini
wachezaji wangu wameniangusha zaidi”. Alisema kocha Malale.
Aidha kocha wa SC Villa Anyau Frank amesema kuwa mechi
ilikuwa sio mbaya kwa sababu kupata ushindi nje ya nyumbani ni muhimu.
“Mechi ya leo sio mbaya kwasababu kupata ushindi nje ya
nyumbani ni kitu muhimu, hata ukienda nje usifungwe ni kitu muhimu, jku
wanapenda sana kupiga chenga, kitu muhimu ni kuona kwamba kuwa na uwezo wa kuzuia
adui kukufunga ni kitu muhimu”. Alisema kocha Anyau.
Katika mchezo wa awali uliochezwa huko Uganda JKU walikubali
kufungwa mabao 4-0 ugenini na leo wakafungwa goli 1-0 katika uwanja wao wa
nyumbani, hivyo JKU wameyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa jumla mabao 5-0.
JKU wamevaa jezi rangi nyekundu na SC Villa wao wamevaa jezi
rangi ya blue.
No comments:
Post a Comment