Thursday, 3 March 2016

Wenger amesema Arsenal iache kuota ndoto za ubingwa.



Jana kocha Wenger alizomewan na mashabiki kwenye uwanja wa Emirates baada ya kufungwa na Swansea. Kwenye moja ya story za jana nilisema kwamba kama Arsenal wakiendelea kuwa na foward butu ambayo haifungi magoli basi ndoto za Arsenal kwenye ubingwa zinaisha mapema.
Kilichotokea jana ni muendelezo wa maneno yale ambapo wachezaji wa Arsenal wameshindwa kufunga na Swansea wametoka na points 3 za ushindi wa 2-1. Baada ya mechi ile Arsenal wamekuwa nyuma kwa points 6 kutoka kwa viongozi wa ligi Leicester City.
Baada ya mechi Wenger alisema “Sipo kwenye mood ya kuongelea mataji usiku huu. Kwa sasa hatutakiwi kuota tena inabidi tuwe wa kweli tu.Nina wasiwasi sana kuhusu matokeo yetu, tumepoteza michezo mitatu na huu ni wakati mgumu sana kwa timu.Haya ni matokeo yanayovunja moyo sana na hali ya wachezaji ipo chini sana”
Arsenal wana mechi ngumu dhidi ya Spurs Jumamosi hii na Wenger aliendelea kusema,“Tuna mechi kubwa tatu zinakuja mbele yetu na tunatakiwa kuendelea kufanya kazi ya msingi na kuonyesha ubora pia.Inabidi turudi nyuma na kufanya kama tulivyokua zamani.Ni bahati mbaya sana usiku wa leo tumetengeneza nafasi lakini tumeshindwa kumalizia”

No comments: